TATIZO LA MTOTO KUHARISHA NA MADHARA YAKE

 KUHARISHA

• • • • •

TATIZO LA MTOTO KUHARISHA NA MADHARA YAKE


Wazazi wengi au Walezi huweza kuona kama kuharisha kwa mtoto ni jambo la kawaida,lakini endapo mtoto ataharisha mfululizo kwa muda wa siku tatu, hii sio jambo la kawaida tena, huweza kuwa ni dalili ya hatari kwa mtoto ambayo huweza hata kuondoa uhai wake.


MADHARA YA MTOTO KUHARISHA MFULULIZO NI PAMOJA NA;


- Mwili wa mtoto kukosa nguvu na kulegemea


- Mtoto kuishiwa na maji ya mwilini


- Mtoto kupoteza maisha yake


MTOTO AMBAYE AMEHARISHA SANA HUWEZA KUONYESHA DALILI HIZI;


- Macho ya mtoto kuingia ndani sana


- Mtoto kukosa nguvu 


- Mwili wa mtoto kulegea sana


- Mtoto kushindwa hata kulia au akilia sauti haitoki vizuri


- Mtoto kuanza kubadilika rangi ya ngozi pamoja na ngozi kuanza kukakamaa


Endapo umeona mtoto ana shida ya kuharisha Mfululizo mpeleke hospital haraka kwa ajili ya kupata matibabu



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!