TATIZO LA MTOTO KUZALIWA NA KICHWA KIDOGO-ANENCEPHALY (Chanzo,dalili,tiba)

AFYA TIPS

• • • • • • 

TATIZO LA MTOTO KUZALIWA NA KICHWA KIDOGO-ANENCEPHALY (Chanzo,dalili,tiba)


Tatizo la mtoto kuzaliwa ni kichwa kidogo sana kuliko kawaida ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Anencephaly ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watoto.


Tatizo hili huhusisha sehemu kubwa ya ubongo wa mtoto au Fuvu la kichwa cha mtoto kutokuwepo au kupungua sana hali ambayo hupelekea mtoto kuonekana ana kichwa kidogo sana kuliko kawaida.


CHANZO CHA TATIZO HILI


shida hii hutokea wakati wa uumbaji wa mtoto hasa sehemu ya kichwani ndipo huu udhaifu hutokea, japo hakuna sababu ya moja kwa moja ya mtoto kuzaliwa na hali hii, ila kuna vihatarishi vya mama mjamzito kuzaa mtoto mwenye shida hii kama vile; 


• Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huathiri uumbaji wa mtoto ikiwa ni pamoja na sehemu ya ubongo.


• Uwepo wa tatizo hili kwenye famia au koo


• Uwepo wa ugonjwa wa kisukari kwa mama mjamzito

N.K


DALILI ZA TATIZO HILI


- Dalili kubwa ya tatizo hili ni mtoto kuzaliwa na kichwa kidogo sana kuliko kawaida huku ikionekana sehemu kubwa ya fuvu la kichwa haipo au imepungua sana.


MADHARA YA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


- Mtoto kuzaliwa akiwa na shida ya kutokuona vizuri


- Mtoto kuzaliwa akiwa na shida ya kutokusikia vizuri


- Mtoto kuzaliwa huku uwezo wake wa kufikiri ukiwa umepungua sana


- Mtoto kuzaliwa na kukua na shida ya kupoteza kumbukumbu

N K


MATIBABU YA TATIZO HILI


✓ kwa bahati mbaya hakuna tiba ya tatizo hili, Hivo mtoto akishazaliwa na shida hii ataendelea nayo kipindi chote cha Maisha yake


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!