COLOR BLINDNESS
• • • • •
TATIZO LA MTU KUSHINDWA KUTOFAUTISHA RANGI(color blindness)
Color Blindness ni tatizo ambalo huhusisha mtu kushindwa kutofautisha rangi anazoziona, na tatizo hili huwaathiri wanaume zaidi ya wanawake.
BAADHI YA SABABU AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA KUTOKEA KWA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
- Hali ya kurithi vinasaba vua tatizo hili katika ukoo au familia flani
- Mtu kupatwa na magonjwa mbali mbali ya macho
- Hali ya kuzeeka sana
- Macho kuingiwa na kemikali ambazo huathiri uwezo wa jicho kuona
- Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huathiri uwezo wa macho kuona vizuri na kuweza kutofautisha rangi
DALILI ZA TATIZO HILI LA MTU KUSHINDWA KUTOFAUTISHA RANGI NI PAMOJA NA;
✓ Mtu kushindwa kutofautisha kati ya rangi ya njano na blue
✓ Mtu kushindwa kutofautisha kati ya rangi nyekundu na kijani
N.K
MATIBABU YA TATIZO HILI LA COLOR BLINDNESS
- Yapo matibabu tu kwa mtu ambaye tatizo hili la kushindwa kutofautisha rangi limetokana na baadhi ya magonjwa ya macho au macho kuingiwa na baadhi ya kemikali,ila vinginevyo hakuna matibabu ya tatizo hili.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LINGINE LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!