TATIZO LA NGOZI KUUNGUA NA KUBADILIKA RANGI BAADA YA KUCHOMWA NA JUA

 NGOZI

• • • • •

TATIZO LA NGOZI KUUNGUA NA KUBADILIKA RANGI BAADA YA KUCHOMWA NA JUA


Watu wengi hupatwa na tatizo hili la ngozi kuungua pamoja na kubadilika rangi kuwa nyekundu baada ya kuchoma na jua, hali ambayo huwatokea watu wengi hasa wanawake na wenye ngozi nyeupe.


CHANZO CHA TATIZO HILI


- Kwa asilimia kubwa hakuna sababu ya moja kwa moja kwanini baadhi ya watu hupatwa na shida hii baada ya kuchomwa na jua,


Lakini wataalam wa afya ya mwili pamoja na magonjwa mbali mbali ya Ngozi, huhusisha tatizo hili na hali ya kinga ya mwili kuanza kuonyesha reaction kwa kuchukulia mionzi ya jua kama kitu cha kigeni kinachotoka kuingia mwilini, hivo kupambana nacho


Hapo ndyo chanzo cha Allergy hii ya ngozi baada ya mtu kuchomwa na jua.


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


- Mtu kuhisi hali ya kuchomwa chomwa kwenye ngozi yake ya mwili


- Ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa nyekundu sana kuliko kawaida


- Hali ya kizunguzungu cha mara kwa mara


- Maumivu makali ya kichwa ambayo yanaenda sambamba na mabadiliko ya rangi ya ngozi


- Wengine hupata maumivu ya tumbo pia kutokana na allergy hii


MATIBABU PAMOJA NA KINGA DHIDI YA TATIZO HILI


- Fanya mambo yafuatayo kujikinga pamoja na kutibu tatizo hili la kwenye ngozi


1. Epuka kukaa kwenye jua kwa muda mrefu


2. Kama kuna ulazima wa kukaa eneo la jua hakikisha unavaa vitu vya kujikinga na jua kama vile; nguo ndefu,mashati ya mikono mirefu,kofia n.k


3. Tumia dawa kama Ibuprofen kama imefikia hatua ya kupata maumivu ambayo huhitaji dawa


4. Hakikisha unapoozesha ngozi ya mwili kwa kuoga mara kwa mara


5. Kunywa maji ya kutosha kwa siku, yaani si chini ya lita 2.5 mpaka 3 ndani ya masaa 24.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!