UTI WA MGONGO
• • • • • • •
TATIZO LA PINGILI ZA UTI WA MGONGO KUBANANA
Tatizo hili la pingili za Uti wa Mgongo kubanana huweza kutokea kutokana na mgandamizo mkubwa pamoja na presha kwenye pingili hizi za Uti wa mgongo,
Ndipo tatizo hili hutokea na kwa baadhi ya watu mgandamizo huu hufikia hatua yakusababisha msuguano mkali,
mpasuko kwenye pingili na hali ya maumivu makali ya Uti wa mgongo.
CHANZO CHA TATIZO LA PINGILI ZA UTI WA MGONGO KUBANANA
Tatizo hili huweza kuchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;
- Pingili za Uti wa mgongo kujipanga vibaya, tatizo ambalo hutokea kwa watu wenye umri mkubwa mfano miaka 60 nakuendelea
- Kubanana kwa pingili za uti wa mgongo kutokana na mgandamizo mkubwa ndani ya uti wa mgongo unaotokana na sababu mbali mbali kama vile; kubeba vitu vizito sana mgongoni
- Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kwenye pingili za uti wa mgongo kama vile; Bacteria,Virusi na Fangasi
- Kuumia sehemu ya mgongoni kwa kudondoka au ajali yoyote ile
- Kupatwa na tatizo la Kansa ya uti wa mgongo iliyoathiri mpaka kwenye pingili za uti wa mgongo
- Pamoja na magonjwa mengine ya mifupa ya uti wa mgongo
DALILI ZA TATIZO LA PINGILI ZA UTI WA MGONGO KUBANANA
✓ Mgonjwa kuanza kupata maumivu makali ambayo huweza kuanzia shingoni,sehemu ya juu ya mgongo na sehemu ya chini ya mgongo
✓ Maumivu makali ya mgongo wakati wa kushiriki tendo la ndoa
✓ Kushindwa kabsa kushiriki tendo la ndoa
✓ Shingo kupatwa na hali ya kukakamaa
✓ Mtu kupatwa na hali ya kuchomwa au kuhisi kuungua moto maeneo mbali mbali kama vile; miguuni na mikononi
✓ Mtu kushindwa kudhibiti utokaji wa mkojo hivo kuweza kupatwa na shida ya kujikojolea
✓ Mtu kupoteza hisia kabsa hasa maeneo ya miguuni
✓ Miguu kuwa dhaifu sana na kushindwa kutembea
✓ Mtu kutembea kwa kuinama
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!