TATIZO LA TUMBO KUNGURUMA NA KUJAA GESI

TUMBO

• • • • • •

TATIZO LA TUMBO KUNGURUMA NA KUJAA GESI


Ni kweli kwamba kila mtu huweza kupitia shida hizi za tumbo kunguruma na kujaa gesi katika vipindi flani vya maisha yake. 


Huku wengine wakiambiana kwamba labda ni kwa sababu ya chakula ulichokula jana,usiku N.K. Na mambo mengine kama haya.


Ukweli ni kwamba sababu kubwa ya tumbo kunguruma au kujaa gesi ni kutokana na kumeza kiwango kikubwa cha hewa tumboni au Chakula kutofanyiwa umeng'enyaji vizuri.


Japo pia kuna baadhi ya vyakula huweza kusababisha kiwango kikubwa cha gesi au hewa tumboni ikiwa ni pamoja na baadhi ya vinywaji kama soda(coca cola) N.K


BAADHI YA SABABU ZA MTU KUJAA GESI TUMBONI PAMOJA NA TUMBO KUNGURUMA NI PAMOJA NA;


1. Kula huku unaongea, tabia hii huweza kusababisha mtu kumeza kiwango kikubwa cha hewa wakati anakula chakula hivo kupelekea tumbo kujaa gesi


2. Ulaji wa chakula kwa haraka haraka sana


3. Unywaji wa kinywaji chochote kwa haraka haraka sana


4. Kuwa na tatizo katika umeng'enyaji wa chakula kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na magonjwa au mashambulizi ya vimelea vya magonjwa ambavyo husababisha chakula kisimeng'enywe vizuri


5. Tabia ya kuvuta sigara huweza kupelekea hewa nyingi kujaa tumboni


6. Mtu kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha mafuta ambayo huchelewa kumeng'enywa


7. Kunywa vinywaji kama Soda ya Coca Cola ambayo husababisha kiwango kikubwa cha gesi tumboni


8. Kula vyakula ambavyo husababisha kiwango kikubwa cha gesi tumboni kama vile; Maharage

N.K


Kumbuka; Mtu ambaye gesi imejaa tumboni huweza kupata shida mbali mbali ambazo huweza kuwa kiashiria kikubwa kwamba Gesi imejaa tumboni kama vile;


- Tumbo kunguruma mara kwa mara


- Mtu kucheua hewa mara kwa mara


- Mtu kutoa hewa kwa Njia ya haja kubwa au Kujamba mara kwa mara


- Wakati mwingine mtu hupata maumivu ya tumbo


- Mtu kupata shida ya kuharisha wakati wa kujisaidia



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!