TATIZO LA UCHOVU WA MWILI USIOISHA(chanzo)

 UCHOVU

• • • • •

TATIZO LA UCHOVU WA MWILI USIOISHA(chanzo)


Katika hali ya kawaida kila mtu kwa namna moja au nyingine huweza kupata uchovu, lakini uchovu ambao hauishi na unakaa kwa muda mrefu huwa sio kawaida ni tatizo, na tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama chronic Fatigue syndrome.


SABABU MBALI MBALI ZA UCHOVU WA MWILI USIOISHA


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuhusishwa na uchovu wa mwili kama vile; mtu kufanya kazi nyingi na kazi zito sana kwa siku husika, 


Lakini endapo uchovu hauishi kabsa ni tatizo na tatizo hilo huweza kusababishwa na sababu zingine mbali mbali kama vile; 


✓ Mtu kupatwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile; Malaria, UTI, magonjwa ya mfumo wa hewa au mfumo wa upumuaji, Matatizo ya moyo N.k


✓ Kuwa na shida kwenye vinasaba vya mgonjwa ambapo kwa mtu huyu shida huanzia tangia anazaliwa


✓ Shida katika mfumo mzima wa kinga ya mwili 


✓ Kuwa na tatizo la msongo wa mawazo kwa muda mrefu


✓ Mwili wako kukosa nguvu ya kutosha kutokana na ukosefu wa chakula cha kutosha kinachozalisha nguvu au shida katika umeng'enyaji pamoja na ufyozwaji wa chakula mwilini


✓ Magonjwa mbali mbali ya mfumo wa chakula

N.k


MATIBABU YA TATIZO HILI LA UCHOVU AMBAO HAUISHI


-Matibabu ya shida hii hutegemea na chanzo chake kama nilivyokwisha kueleza hapo juu,


Hivo basi kama una shida ya uchovu ambao hauishi kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya msaada zaidi ikiwa ni pamoja na vipimo na matibabu sahihi kwako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!