TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI KUTOKANA NA UKOSEFU WA MADINI CHUMA(iron deficiency anemia)
UPUNGUFU WA DAMU
• • • • •
TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI KUTOKANA NA UKOSEFU WA MADINI CHUMA(iron deficiency anemia)
Iron deficiency anemia ni shida au tatizo la upungufu wa damu mwilini unaotokana na ukosefu wa madini chuma yakutosha.
Je kwanini ukosefu wa madini chuma huweza kusababisha upungufu wa damu mwilini?
Madini chuma ndyo hutumika katika utengenezaji au uzalishaji wa seli nyekundu za damu yaani Red blood cells,
hivo upungufu wa madini chuma ni upungufu wa seli nyekundu za damu(red blood cells) na matokeo yake ni upungufu wa damu mwilini.
BAADHI YA SABABU AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA UPUNGUFU WA MADINI CHUMA MWILINI
- Kula mlo au chakula chenye ukosefu wa madini chuma kwa muda mrefu
- Tatizo la mtu kupoteza kiasi kikubwa cha damu mwilini kutokana na sababu mbali mbali kama vile; ajali N.k
- Hali ya mwanamke kuwa mjamzito huweza kusababisha upungufu wa madini chuma
- Tatizo la mwili kushindwa kumeng'enya chakula vizuri na kufyoza madini ya chuma kwenye damu
DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI NI PAMOJA;
• Kupata uchovu wa mwili usio wakawaida
• Mwili kukosa nguvu na kulegemea
• Rangi ya macho,viganja vya mikono,Lips za mdomo kubadilika na kuwa na weupe au Paleness
• Mgonjwa kupata maumivu ya kifua wakati wa upumuaji
• Kukosa pumzi au kupata shida ya upumuaji
• Kupata hali ya kizunguzungu na kupepesuka
• Kupata maumivu makali ya kichwa
N.K
MATIBABU YA TATIZO LA UKOSEFU WA DAMU MWILINI
✓ Shida hii huweza kutibika kulingana na chanzo cha tatizo kwa kutumia njia mbali mbali kama vile;
Mgonjwa kuwekewa damu na kudhibiti kiwango cha damu kilichopotea mwilini
Mgonjwa kupewa dawa mbali mbali zinazoongeza kiwango cha madini chuma mwilini kama vile FEFOL kwa wajawazito
Ulaji wa vyakula vinavyoongeza damu kama vile mboga za majani jamii ya matembele N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!