MFADHAIKO
• • • • •
UGONJWA WA DEPRESSION(mfadhaiko)
Ugonjwa huu huweza kumpata mtu yeyote bila kujali umri wala kazi au heshima aliyokuwa nayo.
Ugonjwa huu huhusisha mtu kuwa na huzuni iliyopita kiasi na mawazo mengi hali ambayo humfanya hata ashindwe kufanya kazi zake za kila siku.
CHANZO CHA UGONJWA WA DEPRESSION(MFADHAIKO)
Tafiti za Wataalam wa afya husema kwamba hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huhusishwa na kutokea kwa tatizo hili, bali huweza kuwa mkusanyiko wa sababu nyingi ndiyo hupelekea mtu kupatwa na shida hii.
Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na;
- Hali mbaya ya kiuchumi ya mhusika mwenyewe
- Matatizo mbali mbali ya Kifamilia ikiwa ni pamoja na migogoro ndani ya familia
- Kufiwa gafla na mtu wako wa karibu ambaye alikuwa tegemezi kwako kwa kila kitu
- Kuwa na shida katika mahusiano ya kimapenzi
- Kufukuzwa kazi kwa wewe ambaye ulikuwa umeajiriwa
- Kupigwa, Mimba yako kukataliwa na aliyekupa mimba N.K
DALILI ZA UGONJWA WA DEPRESSION AU MFADHAIKO NI PAMOJA NA;
- Mtu kuanza kuongea mwenyewe
- Kulia mwenyewe bila watu kujua sababu ya msingi inayokufanya ulie
- Kufanya kazi ndogo lakini kwa kutumia muda mwingi sana
- Kuongea mambo ambayo hayapo au hayawezekani kwa hali ya kawaida
- Kuongea habari za kutaka kujiua mara kwa mara au kumuua mtoto wako uliyemzaa mwenyewe
- Kuwa mtu wa kutumia muda mwingi kwa ajili ya kulala
TIBA YA UGONJWA HUU WA MFADHAIKO
- Kuna njia mbali mbali ambazo hutumiwa kumsaidia mtu mwenye tatizo hili kama vile;
Matumizi ya dawa maalumu
Kukutana na wanasaikolojia
Kujichanganya na watu na kuacha kukaa peke yake
kuashuriwa kuanza kuwa mtu wa kufanya mazoezi ya mwili sana na michezo mbali mbali unayoipenda kama mpira wa miguu N.K
Kuangalia movies kama wewe ni mpenzi wa movies
Kwenda ibadani, Msikitini au kanisani kulingana na imani yako
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!