DONDAKOO
• • • • •
UGONJWA WA DONDAKOO(chanzo,dalili na tiba yake)
Ugonjwa wa dondakoo ni ugonjwa ambao humpata mtu baada ya kushambuliwa na bacteria ambao kwa kitaalam hujulikana kama Corynebacterium Diphtheria.
Mtu huweza kupata bacteria hawa kwa njia mbali mbali kama vile; Kugusa kitu chochote ambacho kimeshikwa na mgonjwa wa dondakoo au kwa njia ya kugusana naye moja kwa moja.
DALILI ZA UGONJWA WA DONDAKOO NI PAMOJA NA;
- Joto la mwili la mgonjwa kupanda juu kuliko kawaida au mgonjwa kuwa na homa
- Mgonjwa kupata tatizo la kutokuona vizuri
- Ngozi ya mwili kwa mgonjwa kubadilika rangi na kuwa na rangi mithili ya rangi la blue
- Kuhisi baridi mwilini kuliko kawaida
- Kuwa na shida ya kuvimba na kuumwa kwa tezi maeneo ya shingoni
- Mgonjwa kupatwa na vidonda maeneo ya kooni ndyo maana ya jina la Dondakoo likatokea hapo
WATU WALIOPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA DONDAKOO
1. Watu wanaotumia muda mwingi kukaa sehemu ambazo kuna mikusanyiko mikubwa ya watu kama vile; sokoni,stend N.K
2. Watu ambao wanakaa kwenye mazingira machafu sana
3. Watu ambao wanaumwa magonjwa ambayo husababisha kinga ya mwili kuwa chini sana, Mfano; Wagonjwa wa TB, Ukimwi N.K
4. Watu ambayo hawakupata chanzo maalumu ya kuzuia ugonjwa huu wa Dondakoo inayojulikana kwa jina la DTP
MATIBABU YA UGONJWA WA DONDAKOO
- Matibabu ya ugonjwa dondakoo huhusisha matumizi ya dawa za aina mbali mbali kama vile; Penicillin, Erythromycin N.K
Hivo ni muhimu kwenda hosptal au kuongea na wataalam wa afya ili kupata tiba sahihi pamoja na dose sahihi kulingana na tatizo lako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!