HAEMOPHILIA
• • • • • •
UGONJWA WA HAEMOPHILIA(chanzo,dalili pamoja na tiba yake)
Ugonjwa wa haemophilia ni ugonjwa ambao huhusisha damu kushindwa kuganda kama ilivyokawaida, huku chanzo chake kikubwa kikiwa ni ukosefu wa protein muhimu kwa ajili ya kusaidia damu kuganda maarufu kama BLOOD-CLOTTING FACTOR.
DALILI ZA UGONJWA WA HAEMOPHILIA NI PAMOJA NA;
1. Kuvuja damu nyingi sana baada ya kupata kijeraha kidogo tu mwilini
2.Kwa mwanamke, huweza kuvuja damu nyingi sana na ambayo huchukua muda mrefu kukata wakati wa hedhi
3. Damu kuendelea kutoka baada ya kufanyiwa upasuaji
4. Kuvuja damu nyingi hata baada ya kung'olewa jino
5. Damu kutoka wakati wa kukojoa au wakati wa kujisaidia haja kubwa
6. Kupatwa na maumivu makali ya viungo,misuli, pamoja na joints
7. Kupatwa na hali ya kizunguzungu kikali
8. Mwili kukosa nguvu pamoja na kuchoka sana
9. Kuanza Kuvuja damu puani bila sababu ya Msingi au yakueleweka
10. Kupatwa na maumivu makali ya kichwa
N.K
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA HAEMOPHILIA
- Kwa asilimia kubwa watu ambao wapo kwenye hatari ya kupatwa na ugonjwa wa Haemophilia ni wale ambao wapo kwenye familia au Koo ambayo kuna mtu mwenye tatizo hili.
- Watu wanaotumia dawa za kusababisha damu isigande kwa sababu moja au nyingine.
MADHARA YA UGONJWA WA HAEMOPHILIA NI PAMOJA NA;
- Kuvuja damu nyingi na kupoteza kiasi kikubwa cha damu mwilini
- Kizunguzungu
- Maumivu makali ya kichwa
- Kifo
- Kuwa katika hatari ya kupata maambukizi mengine ya magonjwa
N.K
MATIBABU YA UGONJWA WA HAEMOPHILIA
- Kuna matibabu mbali mbali ya ugonjwa wa haemophilia huku baadhi yakihusisha matumizi ya dawa mbali mbali kama vile;
Desmopressin ambayo husaidia kusisimua na kuongeza uzalishaji wa Protein yaani clotting factor ambayo ndyo muhimu sana katika kusaidia damu kuganda.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!