AFYA YA MIFUGO
• • • • • •
UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE(afya ya mifugo)
Ugonjwa huu wa homa ya nguruwe umeua nguruwe wengi sana na kwa haraka zaidi kuliko magonjwa mengine katika maeneo mbali mbali ya dunia.
NB; Ugonjwa huu wa homa ya nguruwe hushambulia na kuathiri zaidi maeneo haya katika mwili wa nguruwe; Mfumo mzima wa damu, Mfumo wa chakula, pamoja na Mfumo wa upumuaji.
DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE NI PAMOJA NA;
1. Joto la mwili wa nguruwe kuwa juu sana au nguruwe kuwa na homa
2. Nguruwe kukosa kabsa appetite ya chakula, hivo hata ukimpa chakula nguruwe hataki kula
3. Vifo vya gafla kwa nguruwe wengi
4. Nguruwe kunyong'onyea sana
5. Nguruwe kutoa damu kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wake kama vile masikioni,puani N.K
6. Nguruwe kulala lala kila mara
7. Nguruwe kupata shida ya upumuaji
8. Rangi ya ngozi kwa nguruwe kubadilika na kupauka zaidi
9. Nguruwe kuharisha kinyesi kilichochanganyika na damu
10. Eneo la matakoni kubadilika rangi na kuwa jekundu zaidi
11. Nguruwe kupatwa na hali ya kikohozi kila muda
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!