UGONJWA WA HYPERTROPHIC CARDIOMYOPATHY

MOYO
• • • • •
UGONJWA WA HYPERTROPHIC CARDIOMYOPATHY


Ugonjwa wa hypertrophic cardiomyopathy ni ugonjwa wa moyo ambao huathiri sana misuli ya moyo na kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi zake kama kawaida, ikiwa ni pamoja na kazi ya moyo kusukuma damu katika maeneo mbali mbali ya mwili wa binadamu.


Ugonjwa huu kwa asilimia kubwa husababisha misuli ya moyo kuvimba na kuwa mikubwa hasa maeneo ya chemba za Ventricles ndani ya moyo.


CHANZO CHA UGONJWA WA HYPERTROPHIC CARDIOMYOPATHY


Hakuna sababu ya moja kwa moja iiliyotambuliwa kusababisha mtu kupatwa na Ugonjwa huu wa moyo. Ila kuna Baadhi ya sababu mbali mbali zimeonekana kuchangia kuwepo kwa tatizo hili, na sababu hizo ni pamoja na;


1. Mtu kurithi baadhi ya vinasaba vya tatizo hili katika koo au familia flani.


2. Kuzeeka au mtu kuwa na umri mkubwa sana


3. Kuwa na magonjwa mengine mbali mbali ya moyo


4. Kuwa na tatizo la Presha au Shinikizo la damu

N.K



DALILI ZA UGONJWA WA HYPERTROPHIC CARDIOMYOPATHY


• Kupata maumivu ya kifua wakati wa kuvuta na kutoa hewa

• Kupata shida ya upumuaji


• Mgonjwa kukosa pumzi kabsa


• Mgonjwa kuchoka sana


• Mgonjwa kukosa fahamu au kuzimia



TIBA YA UGONJWA WA HYPERTROPHIC CARDIOMYOPATHY


Matibabu ya ugonjwa huu huhusisha matumizi ya njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na; kumuweka mgonjwa sehemu yenye hewa ya kutosha,


Kumpa mgonjwa hewa ya oxygen, Kumlaza mgonjwa kwa kumuinua kidogo kichwa chake,


 pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali kama vile beta-blockers na calcium channel blockers ambazo hufanya kazi ya relax Misuli ya Moyo pamoja na kuruhusu kufanya kazi vizuri ya kusukuma damu.



WATU WALIOPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA HYPERTROPHIC CARDIOMYOPATHY


- Waliopo kwenye familia ambayo kuna mgonjwa wa tatizo hili

- Wazee

- Walevyi wa pombe

- Watu wenye magonjwa mengine ya moyo

- Watu wenye ugonjwa wa Presha au shinikizo la damu


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!