GOUT
• • • •
UGONJWA WA JONGO(Gout,chanzo chake,dalili pamoja na tiba)
Ugonjwa wa jongo au kwa jina lingine Gout, ni ugonjwa ambao huhusisha maumivu pamoja na uvimbe kama virungu kwenye maeneo mbali mbali ya joints za mwilini; Mfano kwenye Miguu pamoja na mikono.
CHANZO CHA UGONJWA WA JONGO AU GOUT
- Ugonjwa huu wa jongo au ugonjwa wa gout husababishwa na uwepo wa kiwango kikubwa cha Uric acid kwenye Damu, na baadae mgonjwa kuanza kupata dalili mbali mbali ikiwemo hii ya virungu au viuvimbe kwenye joints za miguuni na mikononi.
DALILI ZA UGONJWA WA JONGO AU UGONJWA WA GOUT NI PAMOJA NA;
- Kupata maumivu makali kwenye joints za viungo mbali mbali kama vile miguu au mikono
- Kutokewa na viuvimbe kama virungu kwenye joints za miguuni au mikononi pamoja vidole vyake
- Joto la mwili kupanda au mgonjwa kuwa na homa
- Ngozi ya kwenye joints kubadilika rangi na kuwa nyekundu kuliko kawaida
WATU WALIOPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA GOUT
• Wanywa pombe kupita kiasi
• Watu wanaopenda kula nyama sana kama vile nyama ya mbuzi N.K
• Watu wenye ugonjwa wa Sukari
• Watu wenye matatizo ya Figo
• Watu wanene au wenye uzito mkubwa kupita kiasi
• Watu wenye tatizo la Kansa ya kwenye Damu
• Watu wanaotumia dawa zozote zinazohusisha kuongeza kiwango cha Uric acid kwenye damu
• Au watu wenye matatizo mengine yanayohusu damu
MATIBABU YA UGONJWA WA JONGO AU GOUT
- Matibabu ya ugonjwa huu wa jongo au Gout huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali ikiwa ni za vidonge pamoja na sindano.
Zipo dawa za kutuliza maumivu ambayo mgonjwa huyapata kama vile Ibrufen, lakini pia kuna dawa zingine jamii ya Antinflammatory (Corticosteroids) huweza kutumika sana kwa mtu mwenye ugonjwa huu wa gout.
MAMBO YA KUEPUKA ILI KUJIKINGA NA UGONJWA HUU WA GOUT
✓ epuka matumizi ya pombe kupita kiasi
✓ epuka matumizi ya nyama kwa kiwango kikubwa sana
✓ hakikisha unakuwa na uzito wa mwili usiozidi na kuepuka unene uliopitiliza kwa kufanya mazoezi mbali mbali ya mwili pamoja na njia nyingine za kupunguza unene
✓ epuka matumizi ya dawa zinazochochea ongezeko la kiwango kikubwa cha uric acid kwenye damu kama inawezekana
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!