UGONJWA WA KUVIMBA MFUMO WA CHAKULA(inflammatory bowel disease)

 MFUMO WA CHAKULA

• • • • •

UGONJWA WA KUVIMBA MFUMO WA CHAKULA(inflammatory bowel disease)


Kuvimba kwa mfumo wa chakula ni ugonjwa ambao huhusisha kutokea uvimbe kwenye baadhi ya maeneo ya mfumo mzima wa chakula ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Inflammatory bowel disease.


CHANZO CHA UGONJWA HUU


- Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huhusishwa na kutokea kwa ugonjwa huu japo zipo sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili,sababu hizo ni kama vile;


✓ Umri mkubwa


✓ Matumizi ya sigara


✓ Matumizi ya baadhi ya dawa


✓ Kuwa na vinasaba vya tatizo hili katika ukoo au familia 


✓ Tatizo la unene au uzito kupita kiasi


DALILI ZA UGONJWA JUU WA KVIMBA KWENYE MFUMO WA CHAKULA NI PAMOJA;


- Uzito wa mwili kuanza kushuka kwa haraka sana


- Kupata shida ya kichefu chefu pamoja na kutapika


- Kupata shida ya kuharisha,huku kinyesi kikichanganyika na damu


- Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya kula chakula


- Mwili kuchoka kupita kawaida


- Mgonjwa Kupata maumivu makali ya tumbo


MATIBABU YA UGONJWA HUU


- Matibabu ya ugonjwa huu huhusisha matumizi mbali mbali ya dawa kama vile;


• Dawa za kuondoa uvimbe jamii ya Corticosteroids


• Dawa za kudhibiti kinga ya mwili maarufu kama Immuno suppressors


• Matibabu mengine ya dawa jamii ya antibiotics au dawa zingine mbali mbali mfano Metronidazole au flagyl N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!