LIPOMA
• • • • •
UGONJWA WA LIPOMA(chanzo,dalili na tiba yake)
Ugonjwa wa Lipoma ni ugonjwa ambao hutokana na kuzidi kukua kwa Seli hai za mafuta mwilini yaani kwa kitaalam hujulikana kama Fatty Cells na kusababisha Uvimbe kutokea chini ya Ngozi.
Uvimbe huu huweza kuwepo chini ya Ngozi katika maeno mbali mbali ya mwili wa Mgonjwa kama vile; Usoni, Mgongoni,shingoni,Mabegani N.K
CHANZO CHA UGONJWA WA LIPOMA
- Ugonjwa wa Lipoma hutokana na kuzidi kukua kuliko kawaida kwa seli za mafuta mwilini yaani Fatty cells hali ambayo husababisha uvimbe kutokea chini ya Ngozi.
Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huhusishwa na kusababisha hali hii japo kuna sababu ambazo huhisiwa kama vile;
✓ Kurithi vinasaba vya ugonjwa huu wa Lipoma. Mtu ambaye yupo kwenye familia au koo ambayo kuna mgonjwa wa Lipoma huwa katika hatari ya yeye kuwa na tatizo hili pia.
✓ Uvimbe unaotokea chini ya ngozi kutokana na mtu kuumia N.k
DALILI ZA UGONJWA WA LIPOMA NI PAMOJA NA;
- Mtu kuwa na kitu kama kinundu au mpira kwenye maeneo tofauti ya mwili wake, Kinundu hiki ukikishika husogea chenyewe ila hakina maumivu yoyote
(Tazama mfano kwenye picha hapo chini)
MATIBABU YA UGONJWA WA LIPOMA
Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kutibu tatizo hili ila Njia kubwa ni mgonjwa kufanyiwa upasuaji mdogo na kutolewa hicho kinundu chake.
Na mgonjwa kupewa dawa za kuzuia maumivu pamoja na maambukizi ya magonjwa mengine.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!