Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA LUPUS CHANZO CHAKE,DALILI PAMOJA NA MATIBABU YAKE



  LUPUS

• • • • • •

UGONJWA WA LUPUS CHANZO CHAKE,DALILI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Ugonjwa wa Lupus ni ugonjwa ambao chanzo chake ni Mfumo mzima wa kinga ya mwili, Mfumo huu wa kinga ya mwili badala ya kuhusika na kulinda mwili kama lilivyo lengo lake kuu, huanza kushambulia mwili wenyewe.

Miongoni mwa waathirika wa kubwa wa ugonjwa huu wa Lupus ni jinsia ya Kike kuliko wanaume.

DALILI ZA UGONJWA WA LUPUS NI ZIPI?

Ugonjwa wa Lupus huweza kuonyesha dalili halafu baada ya mda dalili zikapotea kabsa, alafu zikarudi tena hapo baadae.

 Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na;

1. Mgonjwa kupata vipele maeneo mbali mbali ya mwili kama vile usoni

2. Kuwa na tatizo la kupungua uzito wako wa mwili kwa kasi sana

3. Mwili kuchoka kupita kiasi na kukosa nguvu

4. Joto la mwili kupanda/kuwa juu au Mgonjwa kupata homa

5. Mgonjwa wa Lupus huweza kupata maumivu ya misuli,joint pamoja na viungo mbali mbali vya mwili

6. Mgonjwa kupatwa na hali kama ya mwili kutetemeka au kutingishwa

7. Kuwa tatizo la kukosa hamu ya kula chakula

8. Mgonjwa kuwa na tatizo la kuishiwa na damu

9. Ngozi kubadilika rangi katika maeneo mbali mbali ya mwili na kuwa nyekundu Mfano; kwenye Mikono

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA LUPUS

- Hakuna tiba ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Lupus,bali kuna tiba ya kudhibiti dalili zinazosababishwa na ugonjwa wa Lupus, 

Mfano; Kama Mgonjwa ataonyesha dalili za mwili kutetemeka atapewa dawa za kuzuia hali hyo, kama anapata maumivu sana,atapewa dawa za kuzuia hali ya maumivu N.K,

 lakini moja ya tiba muhimu huhusisha mgonjwa kupewa dawa ya kupunguza kinga ya mwili kama kinga ya mwili ipo juu sana.

WATU WALIOPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA LUPUS

- Ni pamoja na wanawake, kwani zaidi ya asilimia 80% Wanaopata tatizo hili ni Wanawake

- Watu wenye kinga kubwa ya mwili

- Watu wanaotumia dawa zinazohusiana na kupandisha kwa kiasi kikubwa kinga ya mwili

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments