ANOREXIA NERVOSA
• • • • • •
UGONJWA WA MTU KUTOTAKA KULA(anorexia nervosa)
Ugonjwa wa anorexia nervosa huhusisha swala la mtu kutotaka kula kabsa, kupungua sana uzito kuliko kawaida, huku mtu huyo akihofia kuongezeka uzito kupita kiasi wakati hana uzito huo, (mfano kwenye picha hapo chini; mtu mwembamba sana lakini anajiona mnene kweli)
Hivo watu wenye ugonjwa huu wa Anorexia nervosa hudhibiti sana kiwango cha chakula wanachokula, hata wakati mwingine kujinyima kabsa wakihofia kuwa wanene na uzito mkubwa
CHANZO CHA UGONJWA HUU
- Hakuna sababu ya moja kwa moja ya mtu kupata tatizo hili, ila kuna baadhi ya sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili kama vile;
1. Swala la kigenetics; Kuwa na shida kwa baadhi ya vinasaba vya mwili
2. Mtu kubadilisha mazingira gafla na kuwa mazingira ya kigeni sana
3. Swala la kuwa na tatizo la kisaikolojia
4. Mabadiliko ya gafla ya vichocheo mwilini
5. Mtu kuwa na hofu ya kuongezeka uzito pamoja na madhara yake
DALILI ZA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;
- Mtu kukonda sana
- Mtu kutokula chakula kabsa au kula chakula kiwango kidogo sana mara kwa mara
- Uzito wa mwili kuwa mdogo kupita kawaida
- Mtu kuchoka sana kupita kawaida
- Mtu kuwa na shida ya kiwango kidogo cha damu mwilini
- Kupatwa na kizunguzungu sana
- Kuwa na dalili zote za kuishiwa na maji ya mwili kama vile; macho kuingia ndani, ngozi ya mwili kukakamaa n.k
- Kuwa na shida ya kupoteza fahamu na kuzimia
- Kuwa na tatizo la kukosa usingizi
- Nywele kuwa dhaifu,nywele kunyonyoka zenyewe n.k
-Mwanamke kuwa na tatizo la kutokuona siku zake za hedhi
- Vidole kubadilika rangi na kuwa na rangi ya blue
- Kuvimba miguu na mikono
- Kuwa na shida ya presha kushuka kuliko kawaida
- Kupata choo kigumu na kwa shida sanaa
- Kupata maumivu makali ya tumbo
- Mtu kukwepa kula chakula mbele za watu
- Mtu kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi
N.k
MATIBABU YA UGONJWA HUU
- Hakuna dawa za moja kwa moja kwa ajili ya kutibu tatizo hili, japo kuna dawa za kudhibiti dalili za ugonjwa huu pamoja na mgonjwa kuwa karibu na uangalizi wa wataalam wa afya, kupata tiba ya Kisaikolojia yaani psychotherapy N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!