UVIMBE
• • • • •
UGONJWA WA OVARIAN CYSTS(maana yake,chanzo,dalili,tiba)
Ugonjwa wa Ovarian cysts ni ugonjwa unaohusisha kutokea kwa viuvimbe kwenye vifuko vya mayai yaani Ovaries.
Uvimbe huu unaweza kutokea upande mmoja wa Ovary au sehemu zote mbili, yaani ovary ya kushoto pamoja na ovary ya kulia.
CHANZO CHA UGONJWA WA OVARIAN CYSTS
- Hakuna sababu ya moja kwa moja ya mtu kupata shida hii ya viuvimbe kwenye vifuko vya mayai yaani Ovarian cysts. Ila kuna baadhi ya Sababu hatarishi ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupatwa na shida hii. Sababu hizo ni kama vile;
✓ Matumizi ya dawa ambazo zinahusiana na kuongeza kwa kiwango kikubwa vichocheo vya mwili
✓ Matumizi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha mafuta
✓ Kuwa na tatizo hili kipndi cha nyuma,uwezekano wa kurudi tena kama hukupata tiba sahihi ni mkubwa
✓ Kuwa na shida ya uvimbe kwenye kuta za ndani za mji wa mimba yaani Endometriosis
✓ Kuwa na tatizo la maambukizi kwenye via vya uzazi yaani Chronic Pelvic Infection
✓ Lakini kwa wengine viuvimbe hivi huweza kutokea kipindi yai linatolewa kutoka kwenye vifuko vya mayai.
N.K
DALILI ZA TATIZO LA OVARIAN CYSTS
- Mwanamke kupata maumivu makali chini ya kitovu
- Mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Mwanamke kupata period isiyoeleweka
- Kupata maumivu ya kiuno na mgongo
- Kutokwa na damu ya matone ukeni
- Kuhisi kichefuchefu na kutapika
- Maumivu makali ya kiuno,mgongo au nyonga baada ya kufanya kazi ngumu au kazi za kuinama sana
- Mwanamke kushindwa kushika mimba
- Maumivu ya matiti sana
- Maumivu makali sana ya tumbo wakati wa hedhi, hadi wengine kufikia hatua ya kulazwa hospitalin
MATIBABU YA UGONJWA WA OVARIAN CYSTS
- Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kutibu shida hii ikiwa ni pamoja na njia ya kutumia dawa mbali mbali pamoja na Mgonjwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa viuvimbe hivi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!