UGONJWA WA TAUNI AU PLAGUE(chanzo,dalili na tiba)

 TAUNI

• • • • • •

UGONJWA WA TAUNI AU PLAGUE(chanzo,dalili na tiba)


Ugonjwa wa tauni ni ugonjwa ambao huwapata na kuwashambulia binadamu,panya  lakini na wanya wengine pia, ugonjwa huu kwa kitaalam hujulikana kama Plague.


CHANZO CHA UGONJWA WA TAUNI(PLAGUE)


- Ugonjwa wa tauni ni ugonjwa ambao husababishwa na Bacteria jamii ya Yersinia Pestis ambao wapo kwenye sehemu nyingi mbali mbali duniani.


DALILI ZA UGONJWA AA TAUNI NI PAMOJA NA;


✓ Mgonjwa kupata shida ya upumuaji


✓ Mgonjwa kuwa na mitoki au kuvimba kwa tezi mbali mbali mwilini


✓ Joto la mwili la Mgonjwa kuwa juu au Mgonjwa kuwa na homa


✓ Mgonjwa kupata hali ya kichefuchefu na kutapika


✓ Mgonjwa kupatwa na maumivu makali ya kichwa mara kwa mara


✓ Mgonjwa kupata uchovu sana mwilini


✓ Mgonjwa kuhisi hali ya baridi sana


✓ Mgonjwa kupata maumivu ya joint,viungo na misuli ya mwili


✓ Kuwa na tatizo la kuvuja damu mara kwa mara


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA TAUNI


- Wafugaji


- Watu ambao wanakaa maeneo ambayo kuna idadi ya panya wengi


- Wenye upungufu wa kinga mwilini


MATIBABU YA UGONJWA WA TAUNI


- Ugonjwa wa tauni huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali ikiwa ni pamoja na dawa jamii ya Antibiotics, Hivo kama una dalili hizi au una ugonjwa huu wa tauni ni vizuri kwenda kupata tiba


- Ugonjwa huu huweza kuambukiza mtu mmoja kwenda kwa mwingine,hivo wagonjwa wa tauni huweza kutengwa na kuwa chini ya usimamizi maalum


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!