MTOTO
• • • • •
UKUAJI WA MTOTO(dondoo)
Kuna vitu vya msingi ambavyo hupaswa kuzingatiwa katika kuhakikisha mtoto anakuwa katika afya iliyo bora.
Ukuaji wa mtoto hutegemea lishe pamoja na kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali ambayo huweza kudhoofisha mwili wake pamoja na ukuaji wake.
Kwa mtoto ambaye ukuaji wake hauridhishi huweza kuchelewa sana kwenye hatua mbali mbali za ukuaji wake kama vile; kwenye kuanza kutambaa, kukaa, kusimama,kutembea,kuongea,kuota meno N.K
Uzingatiaji wa lishe ni pamoja na kuhakikisha mtoto ananyonya vizuri maziwa ya mama kwa muda wa miezi 6 bila kupewa na vyakula vingine kwa kipindi hiki chote, na baada ya hapo aanze kuchanganyiwa na vitu vingine japo unyonyeshaji wa maziwa ya mama uendelee hadi mtoto atakapofikisha umri wa miaka 2 au 3.
Mtoto kupewa chanjo zote muhimu kama vile; chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu,ugonjwa wa kupooza(Polio), kuharisha, Na magonjwa mengine kama vile kifaduro,pepopunda,homa ya ini N.K
Upimaji wa uzito kwa mtoto pamoja na mahudhurio yote ya kliniki bado ni muhimu sana katika kuangalia maendeleo na ukuaji wake.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!