VIDONDA VYA TUMBO
• • • • • •
USHAURI KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
Habari za muda huu ni matumaini yangu kwamba unaendelea kujifunza,kupata ushauri na kuendelea kupata tiba kuhusu matatizo mbali mbali juu ya afya yako.
Leo nataka nifafanue kidogo kuhusu vitu vya kuepuka kwa Mtu mwenye vidonda vya tumbo, Watu wengi sana wanasumbuliwa na tatizo la vidonda vya tumbo hadi wengine kufikia hatua ya kupata athari mbali mbali kama vile;
- Kutapika matapishi ambayo yamechanganyika na damu
- Kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na damu
- Kulazwa hospitalini
N.K
Watu ambao wana Presha pamoja na vidonda vya tumbo hupata shida zaidi
USHAURI KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
Kwa mtu ambaye ana Vidonda vya Tumbo aepuke mambo haya;
✓ Epuka kukaa na njaa kwa Muda mrefu, jenga tabia ya kula mara kwa mara
✓ Epuka kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha acid
✓ Epuka kutumia kahawa kama wewe ulikuwa mpenzi wa kahawa
✓ Epuka matumizi ya pombe ukiwa na vidonda vya tumbo
✓ Epuka matumizi ya vyakula ambavyo vina kiwango kikubwa cha viungo kama Pilipili
✓ Uvutaji wa Sigara sio salama kwako,acha pia
Zipo dawa mbali bali ambazo hutumiwa na watu wenye vidonda vya tumbo kama vile Omeprazole N.K, Epuka matumizi ya dawa kiholela pasipo maelekezo kutoka kwa wataalam wa Afya
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!