UZAZI
• • • • • •
USISUBIRI UCHANGANYE UCHUNGU(soma makala hii.!! Mama K)
Helou followers.
Naomba leo nigusie juu ya Hili.
Kwanza kabisa kupambana na Kupunguza VIFO VYA WANAWAKE(WAMAMA) VITOKAVYO na UZAZI kitaalamu tunasema MATERNAL MORTALITY,ni JUKUMU la Jamii Nzima yaan wewe jiran,Mume,ndugu na rafiki wa Mama mjamzito na mama mjamzito mwenyewe mna Majukumu Yenu ya Kutelekeza ili Kumpunguzia Huyu mama Mjamzito Asiwe kwenye hatarishi yaan RISK ya Kupoteza UHAI wake kutokana na Uzazi.
Sisi Wataalamu wa Afya Tuna NAFASI YETU PIA TUNAPOMPOKEA HUYU MAMA MJAMZITO AKIJA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA,lakin Pia Hatuwezi kufikisha lengo BILA kusaidiana na JAMII.
Kuna kamsemo kale kamama Mjamzito ambae Siku zake za kujifungua zimefika,Akianza Kupata Uchungu anashauriwa "ASUBIRI VICHANGANYE ili Akija HOSPITALI Asikae SANA". Yaan Akifika tu ASHUSHE MTOTO hapo hapo😀😀👐.
Hii SIO SAHIHI kabisa,Haitakiwi.
Mama Mjamzito Unapokuwa unapata Uchungu unatakiwa uje Hospitalin ili TUFUATILIE uchungu wako kwa uKaribu lakin na kuweza KUJUA kama Unashida yeyote USAIDIWE ili Kuokoa Maisha ya mama na maisha ya Mtoto
Unaweza "SUBIRI VICHANGANYE"
Kumbe
👇👇
? Mtoto ana kitovu shingon ukamchosha bure.
?kumbe mwanao katanguliza mguu au matako akashindwa kutoka
?kumbe kutokana na mshono wako wa zaman kizazi kimechanika unamwaga damu ndani kwa ndani.
?kondo Limeachia kabla ya wakati Unamwaga damu ndani kwa ndani.
Sababu ni NYINGI za kukulazimu mama mjamzito UWE MIKONON mwa wataalamu mara ty unapopata UCHUNGU.
Na wewe mama mjamzito, mama K,Fuata Ushauri unaopewa na wataalam Unapoenda CLINIC acha Kusikiliza Maneno ya MTAANI
By Dr latifa,MD.
Share please.
#USISUBIRIUCHANGANYE
#punguzavifovitokanavyonauzazi
#okoamama
#okoamtoto
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!