VIDONDA VYA TUMBO
• • • • • •
VISABABISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO
Mpaka sasa zipo sababu kuu mbili ambazo ndo zinapelekea mtu kupata vidonda vya tumbo,zipo na sababu zingine lakini hazichangii sana kwenye ugonjwa huu..nitakwenda kuelezea hizo sababu kama ifuatavyo;
MAAMBUKIZI YA BAKTERIA H- PYLORI:Huyu ni bakteria kiboko katika kusababisha vidonda vya tumbo, kimelea huyu humuingia mtu kupitia mdomo ama kwa kula chakula,kunywa maji au kula kitu chochote chenye kimelea h-pylori.. na jinsi huyu kimelea alivyo mjanja mara zote watu huambukizwa katika kipindi cha utoto na anachofanya kimelea huyu,hujichimbia ndani ya ukuta wa tumbo na kuanza kufanya mambo yake...
Huyu bakteria bado ni tatizo huku africa kwani bado hatuna desturi ya kunawa mikono ama usafi wa vyakula,matunda na maji na pia hatuna desturi ya kujicheki afya zetu..
Inakadiriwa kwamba zaidi ya nusu ya watu wanaoishi ulimwenguni wameambukizwa kimelea h-pylori na wengi wao ni waafrica na kwa Tanzania asilimia 70-80 ya wananchi wote wameambukizwa H-pylori..
Ikumbukwe kwamba sasa H-PYOLORI AMETANGAZWA NA SHIRIKA LA AFYA ULIMWENGUNI(WHO) KUA NI KISABABISHI CHA SARATANI NAMBA MOJA(NUMBER 1 CARCINOGEN)
MATUMIZI YA DAWA ZA NSAIDs:Hii ni sababu kuu pili katika visababishi vya vidonda vya tumbo.. matumizi ya dawa za kuondoloea maumivu za kundi la NSAIDs kama ASPIRINI,DICLOFENAC,NAPROXEN,IBUPRUFEN,INDOMETHACINE,COLECOXIB,PIROXICAM,MELOXICAM,vilevile matumizi ya dawa zingine kama clopidogrel,kcl,zolendronic acid nk..Ifahamike kwamba madhara ya matumizi haya ni tu kwa yule ambae anazitumia mara kwa mara ,
yaani akisikia maumivu kidogo tu anakimbilia madawa tajwa hapo juu.. tujihadhari na haya madawa kwani tofauti na vidonda vya tumbo pia huharibu mafigo na mifumo mingine.
VISABABISHI VINGINE VYA VIDONDA VYA TUMBO AMBAVYO NI KWA KIASI KIDOGO NI KAMA IFUATAVYO
Maambukizi ya virusi vya hepesi,CMV,maambukizi ya kaswende ya tumbo,TB ya tumbo,fangasi ya tumbo nk
Matumizi ya dawa za saratani
mionzi
Saratani maalumu ya Tumbo(gastrinoma)
magonjwa ya mafigo,maini,moyo
Cr: @doktamathew
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!