CHANZO CHA CHUCHU KUUMA NA KUTOA DAMU

 TITI

• • • • •

CHANZO CHA CHUCHU KUUMA NA KUTOA DAMU


Tatizo la matiti kukuuma,chuchu kuvimba,kuwa na vidonda,kutoa maji maji,kutoa usaha au damu, ni miongoni mwa matatizo ambayo hutokea kwenye titi,


Lakini katika makala hii tunazungumzia kuhusu chuchu kuuma sana pamoja na kutoa damu, Je hii ni dalili ya ugonjwa gani?


CHANZO CHA CHUCHU KUUMA NA KUTOA DAMU


- Moja ya sababu kuu ya chuchu kuuma sana pamoja na kutoa damu ni tatizo la Saratani ya matiti au kwa kitaalam hujulikana kama Breast cancer.


Mara nyingi mtu mwenye tatizo la Kansa ya Titi au matiti huanza kutoka damu kwenye chuchu ambayo huambatana na;


✓ Maumivu makali ya titi


✓ Chuchu kuingia ndani zaidi


✓ titi moja ambalo limeathiriwa kubadilika umbo na kuwa kubwa kuliko lingine


✓ kuwa na vitu vigumu kwenye titi mithili ya punje ya harage au mchele ambavyo huweza kushikika mpaka maeneo ya kwapani


✓ Titi kuvimba


✓ Ngozi ya titi kubadilika rangi na kuwa nyekundu kuliko kawaida


✓ Titi kuwa na joto zaidi


✓ Na wakati mwingine usaha kuanza kutoka


KUMBUKA; kama una dalili kama hizi wahi hospitalini kwa ajili ya vipimo zaidi pamoja na matibabu,


Kwa sababu matibabu ya kansa katika stage za mwanzoni hutoa matokeo mazuri zaidi ikiwa ni pamoja na kupona kabsa,


Tofauti na ukichelewa sana kupata tiba.


Kujua SABABU za Chuchu Kutoa MAZIWA yenyewe SOMA HAPA..!!


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!