CHANZO CHA MAMA MJAMZITO KUTAPIKA SANA PAMOJA NA TIBA YAKE

 MJAMZITO

• • • • 

CHANZO CHA MAMA MJAMZITO KUTAPIKA SANA PAMOJA NA TIBA YAKE


Tatizo la mama mjamzito kuhisi kichefuchefu na kutapika hujulikana kama Morning sickness,


Tatizo hili hupenda kutokea katika miezi mitatu ya mwanzoni ya ujauzito yaani First trimester hasa wiki ya 9 na kuendelea.


DALILI;


Tatizo la Morning sickness huambatana na dalili mbali mbali kama vile;


- Mama Mjamzito kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika mara kwa mara


- Mama mjamzito kuanza kuhisi harufu za tofauti


- Mapigo ya moyo kwenda mbio


- Mama mjamzito kutema sana mate kupita kiasi.


CHANZO CHA TATIZO HILI


✓ Hakuna sababu ya moja kwa moja kuhusu chanzo cha shida hii,ingawa wataalam wa afya huhusisha tatizo hili na;


• Mabadiliko ya vichocheo vya mwili ambayo hutokea kipindi cha ujauzito


• Lakini pia kwa watu wenye matatizo mengine kama vile; magonjwa ya kwenye tezi la thyroid au magonjwa ya ini


WANAWAKE AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


- Ambao wamewahi kusumbuliwa na tatizo hili kwenye mimba zilizopita


- Ambao husumbuliwa na tatizo la kuhisi kichefu chefu pamoja na kutapika mara kwa mara kabla hata ya kuwa na ujauzito


- Ambao wana mimba ya mapacha au watoto zaidi ya wawili


WAONE WATAALAM WA AFYA ENDAPO;


- unapata kichefuchefu na kutapika kupita kiasi


- unakojoa mkojo mdogo sana pamoja na mkojo kubadilika rangi na kuwa mweusi


- mapigo ya moyo yanabadika,unakosa pumzi,mwili kuishiwa na nguvu,kulegea n.k


- unahisi kizunguzungu kikali au kuzimia


- unaona marue rue 

N.K


MATIBABU YA TATIZO HILI


- zipo dawa mbali mbali ambazo mgonjwa huweza kupewa hospitalini endapo tatizo limezidi kama vile;


• vitamin B6 supplements au pyridoxine


• Doxylamine 

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!