MTOTO
• • • • •
CHANZO CHA MTOTO KUTEMBELEA VIDOLE(toe walking)
Mtoto kutembelea vidole yaani toe walking, mara nyingi ni hali ambayo humtokea mtoto wakati anajifunza kutembea,
Kumbuka; Mtoto kutembelea vidole akiwa na umri wa zaidi ya Miaka 2 huweza kuwa ni tatizo,
Watu wengi hawajui pia kuna baadhi ya matatizo ambayo huweza kuchangia mtoto kutembelea vidole, na matatizo hayo ni kama vile;
✓ Mtoto kupatwa na tatizo la autism
✓ Mtoto kupatwa na matatizo kwenye misuli yake yaani Muscular Dystrophy
✓ Mtoto kuwa na matatizo kwenye ubongo yaani Cerebral palsy
✓ Mtoto kuwa na matatizo kwenye tendons n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI
- Mtoto huweza kukutana na wataalam wa afya na kupatiwa tiba mbali mbali kama vile;
Tiba ya mazoezi yaani Physiotherapy pamoja na Upasuaji kama tatizo litahitaji huduma hii
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!