CHANZO CHA TATIZO LA MAMA KUVUJA DAMU NYINGI BAADA YA KUJIFUNGUA(postpartum hemorrhage-PPH)

 UZAZI

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA MAMA KUVUJA DAMU NYINGI BAADA YA KUJIFUNGUA(postpartum hemorrhage-PPH)


Moja ya matatizo makubwa ambayo huweza kumpata mama baada ya kujifungua na hata wakati mwingine kupelekea kupoteza maisha yake kabsa ni tatizo hili la;


Mama kuvuja damu kupita kiasi baada ya Kujifungua,


Tatizo hili huhusisha mama kuvuja damu kwa wastani wa 500 mls au zaidi, na kwa kitaalam hujulikana kama postpartum hemorrhage au PPH.


CHANZO CHA TATIZO LA MAMA KUVUJA DAMU NYINGI BAADA YA KUJIFUNGUA(postpartum hemorrhage-PPH)



- Mji wa mimba au uterus kushindwa kusinyaa na kurudi katika hali yake ya awali(uterus atony), Sababu ambayo hupelekea mama kuendelea kuvuja damu baada ya kujifungua

- Mama kuwa na mabaki,mabonge mabonge n.k ndani ya mjia wa uzazi hali ambayo hupelekea mama huyu kuendelea kublid sana


- Mama kupata jeraha au mchubuko wowote wakati wa kujifungua


- Mama kupatwa na tatizo la damu kushindwa kuganda yaani kwa kitaalam Coagulopathy

n.k


KUMBUKA, kuna aina mbili za PPH


✓ Kuna primary PPH- ambapo mama huvuja damu sana baada ya kujifungua lakini ndani ya masaa 24


✓ Na kuna Secondary PPH- mama kuvuja damu kupita kiasi kuanzia masaa 24 mpaka kipindi cha ndani ya wiki 6.


MAMA KUVUJA DAMU BAADA YA KUJIFUNGUA NI MOJAWAPO YA DALILI ZA HATARI kwa mama hivo anatakiwa kupata msaada wa haraka sana.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!