CHANZO CHA TATIZO LA MTU KUTAPIKA AKIWA KWENYE GARI

 KUTAPIKA

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA MTU KUTAPIKA AKIWA KWENYE GARI


Tatizo la mtu kupata kichefu chefu na kutapika wakati anasafiri kwa gari,ndege,meli au usafiri wowote sio ugonjwa mkubwa wa kutisha,


japo huweza kukusababisha usifurahie safari yako kila mara unavyosafiri.


CHANZO CHA TATIZO LA MTU KUTAPIKA AKIWA KWENYE GARI


- Tatizo hili husababishwa na mvurugano katika sehemu ya ndani ya sikio(inner ear) hali ambayo hupelekea kukosa uwiano(imbalance) mwilini kati ya unachokiona na unavyojisikia wakati gari likienda,


ndipo matokeo yake mtu huanza kujisikia vibaya,kichwa kuuma sana,kizunguzungu,kichefuchefu pamoja na kutapika. 


MATIBABU YA TATIZO LA KUTAPIKA WAKATI WA SAFARI


- Tatizo hili huisha lenyewe pale tu unapofika au gari linaposimama, japo kwa baadhi ya watu huendelea kujisikia vibaya hata baada ya kufika wanapoenda,


Zipo njia mbali mbali za kumsaidia mtu mwenye tatizo hili kama vile;


- Kula vitu kama Pipi(Ivory), bigjii n.k


- Kuhakikisha anapata hewa ya kutosha wakati wa safari,hivo akae sehemu ya dirishani


- Matumizi ya tangawizi


- Pia kuna matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; 


• Scopolamine


• Promethazine


• Cyclizine


• Meclizine


• Dimenhydrinate

N.K


EPUKA MAMBO HAYA HAPA;


- Epuka kutazama nje jinsi vitu vinavyoenda na kurudi nyuma wakati gari inatembea, tazama vitu ambavyo havitembei


- Epuka kutumia muda mwingi kusoma makala zozote wakati unasafiri


- Epuka kutumia marashi au perfumes zenye harufu kali

N.K


Kujua zaidi kuhusu kuumwa safarini soma hapa..!!!


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!