CHANZO CHA TATIZO LA MWANAUME KUWAHI KUFIKA KILELENI PAMOJA NA TIBA YAKE(premature ejaculation)

 AFYA YA UZAZI KWA WANAUME

• • • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA MWANAUME KUWAHI KUFIKA KILELENI PAMOJA NA TIBA YAKE(premature ejaculation)


Tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni wakati wa kufanya mapenzi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Premature ejaculation huwatokea wanaume wengi,


Na wengi wao huanza kuona tatizo pale ambapo hali hii inapotokea kwa zaidi ya mara moja na kuanza kujiuliza hivi chanzo chake ni nini?


KUMBUKA; Tatizo hili limegawanyika katika sehemu kuu mbili,


• Kuna wanaume tangu waanze kushiriki tendo la ndoa huwahi kufika kileleni kuliko wenza wao,hiyo tunaita Primary premature ejaculation


• Na wengine walikuwa hawana tatizo hili la kuwahi kufika kileleni wakati wa kufanya mapenzi,bali tatizo huanza kutokea ndani ya kipindi flani cha maisha,hii tunaita secondary Premature ejaculation


CHANZO CHA TATIZO LA MWANAUME KUWAHI KUFIKA KILELENI WAKATI AKIFANYA MAPENZI


- Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii, na sababu hizi ni kama vile;


1. Mwanaume kuanza kushiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza


2. Mwanaume kuwa na msongo wa mawazo na kushindwa kudhibiti hisia zake


3. Kukaa kwa muda mrefu bila kufanya mapenzi


4. Mwanaume kuwa na wasi wasi mkubwa wa kumridhisha mwenzake wakati wanafanya mapenzi


5. Mwanaume kuwa na tatizo la uume kushindwa kusimama yaani kwa kitaalam Erectile Dysfunction


6. Mwanaume kuwa na tatizo la Mvurugiko wa vichocheo mwilini hasa vichocheo vya kiume yaani Testosterones


7. Mwanaume kurithi tabia za vinasaba vya tatizo hili


8. Kutokuwa na kiwango sawa cha kemikali zinazozalishwa na ubongo maarufu kama Neurotransmitters


9. Mwanaume kuwa na hitilafu katika mfumo wake wa fahamu au nerves


10. Maambukizi ya magonjwa kwenye tezi la Prostate au Urethra


11. Mwanaume kupata uvimbe kwenye tezi la Prostate au Urethra

N.k


MATIBABU YA TATIZO LA MWANAUME KUWAHI KUFIKA KILELENI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI


- Matibabu ya tatizo hili hutegemea chanzo chake, ila kwa ujumla wake, mwanaume  mwenye shida hii huweza kupewa dawa,huduma ya ushauri,psychotherapy N.k


hivo ni muhimu kuongea na wataalam wa afya ili upate tiba sahihi juu ya tatizo lako 


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!