AFYA TIPS
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA TUMBO KUJAA GESI WAKATI WA BARIDI
Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 87% ya wanawake hupatwa na matatizo mbali mbali kwenye mfumo wa chakula na umeng'enyaji wa chakula kama vile; Tumbo kujaa gesi, kupata choo kigumu n.k
Huku asilimia 63% ya wanawake hawa wakipatwa na tatizo la tumbo kujaa gesi peke yake hasa wakati wa baridi,
Je chanzo cha tumbo kujaa gesi wakati wa baridi ni nini?
CHANZO CHA TATIZO LA TUMBO KUJAA GESI WAKATI WA BARIDI
- Kutokunywa maji ya kutosha wakati wa baridi,
ukweli ni kwamba watu wengi hawanywi maji mengi kipindi cha baridi hali ambayo huweza kuwapelekea kuwa na matatizo kwenye mfumo wa chakula kama vile; chakula kutokufanyiwa umeng'enyaji vizuri, kupata choo kigumu sana, tumbo kujaa gesi n.k
- Pia baadhi ya tafiti zinaonyesha watu wengi huacha kufanya mazoezi na kukaa sehemu moja kwa asilimia kubwa kipindi cha Baridi,
Licha ya hali ya hewa kuwa rafiki sana kwa mtu anayependa kufanya mazoezi, watu wengi hawafanyi mazoezi kipindi cha baridi
Hali hii hupelekea watu kuwa matatizo mbali mbali ya matumbo kama gesi kujaa tumboni n.k kwa kukaa sehemu moja kwa muda mrefu au kulala bila mazoezi baada ya kushiba chakula
- Lakini pia kula chakula kingi kwa wakati mmoja,
Tafiti zinaonyesha kwamba watu wengi huongeza uwezo wao wa kula kipindi cha baridi,
hivo hali ya watu kula chakula kingi kwa wakati mmoja kipindi cha baridi huweza kuchangia matumbo kujaa gesi na matatizo mengine katika mfumo wa chakula na Umeng'enyaji wake
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!