CHOLESTEROL
• • • • • •
CHANZO NA MADHARA YA KIWANGO KIKUBWA CHA CHOLESTEROL MWILINI
Ili mwili uwe katika afya njema pamoja na seli hai za mwili zifanyaje kazi vizuri ni lazima kudhibiti kiwango cha Cholesterol mwilini,
Kiwango kikubwa cha cholesterol mwilini ni chanzo cha magonjwa mbali mbali kama vile; magonjwa ya moyo n.k
CHANZO CHA KUWA NA KIWANGO KIKUBWA CHA CHOLESTEROL MWILINI
- Kuna vyanzo mbali mbali vya mtu kuwa na tatizo la kiwango kikubwa cha Cholesterol mwilini pamoja na watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata tatizo hili;
• Cholesterol husafirishwa kwenye damu ikiwa imeunganishwa na protein hivo kutengeneza kitu kinaitwa LIPOPROTEIN,
Hapa kuna makundi mawili yaani High Density Lipoprotein pamoja na Low density Lipoprotein,
Hivo basi, Kazi kubwa ya High density Lipoprotein(Cholesterol nzuri) ni kusaidia kubeba kiwango cha Cholesterol kilichozidi na kukirudisha kwenye Ini,
Lakini hii Low density Lipoprotein(Cholesterol mbaya) ndyo chanzo cha kuleta matatizo na madhara makubwa mwilini, low density protein husababisha mishipa ya damu ya Arteries kuwa myembamba,kuziba n.k
✓ Watu ambao wapo kwenye hatari ni pamoja na;
1. Wanaokula vyakula ambavyo vina kiwango kikubwa cha mafuta mabaya kama vile; nyama nyekundu n.k
2. Watu ambao wana uzito mkubwa au wanene kupita kawaida
3. Watu ambao hawafanyi mazoezi ya mwili
4. Mtu mwenye umri mkubwa, kwani kadri umri unavyokuwa mkubwa ndipo uwezo wa ini kufanya kazi hupungua na kusababisha ini kushindwa kuondoa kiwango cha Lipopotrein(cholesterol+Protein) kinachozidi mwilini
5. Watu wanaovyuta sigara sana
6. Watu wenye ugonjwa wa Kisukari, kwani ugonjwa huu huongeza kiwango cha cholesterol mbaya mwilini yaani Low density Lipoprotein
MADHARA YA KIWANGO KIKUBWA CHA CHOLESTEROL MWILINI
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!