KIPANDA USO
• • • • • •
Dalili za ugonjwa wa kipanda uso(migraine)
Kipanda uso ni tatizo ambalo huhusisha mtu kupatwa na maumivu makali sana ya kichwa ambayo hutokana na sababu mbali mbali kama vile;
hali ya kutanuka kwa mishipa ya damu kichwani kama vile mishipa aina ya Artery,
mabadiliko ya mfumo wa damu yaani Blood stream na mabadiliko ya vichocheo kama vile; kichocheo aina ya Serotonin ambacho huhusika na kudhibiti kiwango cha maumivu kwenye mfumo wa fahamu.
Vyote hivi huchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;
✓ Mtu kuwa na msongo wa mawazo
✓ Matumizi ya pombe kali kupita kiasi
✓ Kunywa vinywaji vyenye caffeine nyingi kama kahawa N.k
✓ Kukosa muda wa kutosha wa kulala
✓ Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; vidonge vya uzazi wa mpango n.k
✓ mabadiliko ya hali ya hewa mfano; Kuwa na jua kali pamoja na joto sana
N.k
DALILI ZA TATIZO LA KIPANDA USO(MIGRAINE) NI PAMOJA NA;
Siku moja au mbili kabla ya tatizo hili kutokea,mtu huweza kupata mabadiliko kama vile;
• Kuanza kupata choo kigumu
• Kupoteza mood
• Shingo kukakamaa
• Kiu ya maji kuongezeka sana pamoja na mtu kukojoa sana
• Mtu kupiga miayo sana
• Kuanza kupata shida ya kutokuona vizuri au kuona marue rue
NDIPO BAADAE dalili zingine hujitokeza mfano;
- Maumivu makali ya kichwa
- Mshipa kucheza cheza upande mmoja wa kichwani
- Kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
- Mtu kupata kizunguzungu kikali
- Kuhisi sauti za makelele masikioni
- Kupata shida ya kuongea
- Mwili kutetemeka
- Mwili kukosa nguvu
- Dalili za kuchanganyikiwa
N.K
MATIBABU YA TATIZO HILI LA KIPANDA USO
• Zipo dawa mbali mbali za kuondoa maumivu haya kama vile; Ibuprofen, Paracetum N.k
japo endapo mtu hupata dalili mbaya zaidi kama kushindwa kuongea,mwili kutetemeka, n.k ni vizuri kuwaona wataalam wa afya.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!