UZAZI
• • • • •
DAWA AMBAZO HAZIRUHUSIWI KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Nidhahiri kwamba kila dawa ambayo huingia kwenye mzunguko wa damu hupita kwa kiasi flani kwenye maziwa ya mtoto wakati ananyonya kwa mama yake.
Baadhi ya dawa huwa ni salama hazina madhara yoyote na zingine zina viambata vya sumu au kemikali ambazo huweza kuhatarisha afya ya mtoto.
DAWA AMBAZO HAZIRUHUSIWI KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Baadhi ya dawa ambazo haziruhusiwi kwa mama anayenyonyesha ni pamoja na;
- Dawa za uzazi wa mpango zenye rangi mbili yaani Combined oral contraceptives(COC's), kwani huathiri uzalishaji wa maziwa kwa mama anayenyonyesha
- Dawa mbali mbali za kansa yaani anticancerous drugs
- Iodine
- Oral retinoids
- Amiodarone, ambayo huweza kusababisha tatizo la Hypothyroidism kwa mtoto
- Dawa ambazo zipo kwenye kundi la Anticoagulants mfano; Warfarin n.k
matumizi ya dawa hizi kwa kiwango kikubwa huweza kusababisha tatizo la kuvuja damu yaani Hemorhage
- Dawa ambazo zipo kwenye kundi la Cytotoxic drugs mfano; Methotrexate
Dawa hizi huweza kuathiri mfumo wa mmeng'enyo ndani ya mwili wa mtoto, Kushusha kinga ya mwili n.k
- Dawa ambazo zipo kwenye kundi la Psychoactive drugs mfano; Diazepam,Lorazepam,Clozapine n.k
Dawa hivi huweza kuhusishwa la kuleta athari katika mfumo wa fahamu kwa mtoto ikiwa ni pamoja na kuleta matatizo kama vile; Colic, Mtoto kukosa usingizi n.k
- DAWA ZINGINE NI KAMA VILE;
• Bromocriptine, ambayo huweza kuathiri uzalishaji wa maziwa
• Atenolol, ambayo huweza kusababisha mapigo ya moyo kwa mtoto kushuka chini
• Aminosalicylic acid, ambayo huweza kusababisha mtoto kupatwa na tatizo la kuharisha
• Acebutolol, ambayo huweza kusababisha presha kushuka,mapigo ya moyo pamoja na tatizo la kupumua kwa shida
• Sulfisoxazole na Sulfapyridine, dawa hizi mama asinywe endapo mtoto ana tatizo la umanjano yaani Jaundice, G6PD deficiency au kazaliwa kabla ya wakati yaani premature baby
• Dawa jamii ya Corticosteroids,huweza kuathiri ukuaji wa mtoto
• Chloramphenicol, huweza kusababisha tatizo kwenye mifupa ya mtoto
N.k
Kujua Zaidi kuhusu KANUNI za UNYONYESHAJI BORA soma hapa..!!!
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!