FAHAMU KUHUSU BACTERIA Clostridium difficile PAMOJA NA MADHARA YAKE MWILINI
BACTERIA
• • • • •
FAHAMU KUHUSU BACTERIA Clostridium difficile PAMOJA NA MADHARA YAKE MWILINI
Clostridium difficile,huyu ni bacteria ambaye hushambulia sana sehemu ya utumbo mkubwa yaani COLON na kusababisha madhara mbali mbali kama kuharisha n.k
Bacteria huyu huweza kupatikana kwenye mazingira mbali mbali kama vile;
✓ Kwenye udongo
✓ Kwenye maji
✓ Kwenye hewa
✓ Kwenye chakula
✓ Kwenye kinyesi cha binadamu pamoja na Wanyama
MADHARA AMBAYO HUWEZA KUSABABISHWA NA BACTERIA Clostridium difficile MWILINI Ni pamoja na;
- Mtu kupata tatizo la kuharisha sana
- Kuongezeka kwa kiwango cha Seli nyeupe za damu yaani Increase in White blood cells count
- Mtu kupatwa na tatizo la figo kufeli au kushindwa kufanya kazi
- Mtu kuvimba tumbo
- Mtu kupoteza kabsa hamu ya kula
- Uzito wa mwili kushuka kwa kasi zaidi
- Mtu kupatwa na tatizo la maji ya mwili kuisha
- Mtu kupatwa na tatizo la kichefuchefu pamoja na kutapika
- Mtu kuanza kujisaidia kinyesi kilochochanganyika na damu au Usaha
- Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na Homa
- Mtu kupata tatizo la mapigo ya moyo kwenda mbio
- Mtu kuanza kupata maumivu makali ya tumbo pamoja na tumbo kukaza sana
- N.k
KUMBUKA; dalili za maambukizi ya Bacteria Clostridium difficile huanza kuonekana ndani ya siku Moja au miezi miwili baadae,lakini kwa mtu ambaye anatumia dawa(antibiotics) huweza kuanza kupata dalili ndani ya siku 5-10.
• Kwenye utumbo kuna wastani wa seli za bacteria Trillion 100 na mpaka 2,000 kwa idadi ya bacteria Wazuri ambayo hulinda mwili dhidi ya maambukizi mbali mbali,
Hivo basi kuna baadhi ya dawa zikitumiwa huweza kuwaharibu kabsa hawa bacteria wazuri na kusababisha mwili wako kushambuliwa kwa urahisi na Bacteria huyu Clostridium difficile,
Dawa hivo ni kama vile;
- Clindamycin
- Penicillins
- Cephalosporins
- Fluoroquinolones
N.k
VIPIMO;
Mtu mwenye dalili za mashambulizi ya bacteria Clostridium difficile huweza kufanyiwa vipimo mbali mbali, kama kuchukua kinyesi chake n.k
MATIBABU YA MASHAMBULIZI YA Clostridium difficile
- Zipo dawa mbali mbali ambazo huweza kutumika kwa mashambulizi ya Clostridium difficile kama vile;
• Vancomycin
• Metronidazole
• Fidaxomicin
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!