FAHAMU MAMBO 10 KUHUSU CHANJO YOYOTE

 CHANJO

• • • • •

FAHAMU MAMBO 10 KUHUSU CHANJO YOYOTE


1. Lengo kuu la chanjo ni kukukinga usipate ugonjwa Flani, mfano;


 kuna chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu maarufu kama BCG, Kuna chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza au POLIO n.k


2. Sio kila chanjo lazima iwe sindano, kuna chanjo zingine hutolewa kwa njia ya matone mdomoni n.k


3. Chanjo huweza kusababisha joto lako la mwili kupanda kwa muda flani au mtu kuwa na homa;


 kutegemea na aina ya chanjo uliyopewa, kinga ya mwili wako, allergy n.k


4. Hakuna uhusiano katika ya mtoto kupewa chanjo na kuchelewa au kudumaa katika ukuaji wake,


kwani baadhi ya watu wana dhana kwamba chanjo huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwa mtoto kama vile; Autism n.k


5. Magonjwa mengi ambayo husababishwa na Virusi hukingwa kwa Kutumia chanjo


6. Chanjo huweza kusababisha ngozi ya sehemu ilipochomwa kuwa nyekundu kwa muda au kuvimba kidogo


7. Matumizi ya chanjo yamesaidia sana kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo,magonjwa pamoja na ulemavu mbali mbali kwa watu ulimwenguni kote


8. Chanjo sahihi kutumika kwa binadamu ni lazima iwe imefanyiwa utafiti pamoja na majaribio ya kutosha kabla ya matumizi


9. Kuna aina nyingi sana za chanjo ambazo hutolewa kwa watoto wadogo na zingine kutolewa kwa watu wazima


10. Hizi hapa ni baadhi ya chanjo ambazo hutolewa kwa binadamu;


- Kuna chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu maarufu kama BCG


- kuna chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza yaani POLIO


- Kuna chanzo cha kuzuia kuharisha maarufu kama ROTAX


- kuna chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Homa ya Ini maarufu Kama HEPATITIS B VACCINES


- Kuna chanjo ya kuzuia pepopunda au TETENASI


- Kuna chanjo ya kuzuia KICHAA cha Mbwa


- Kuna chanjo ya Kuzuia  magonjwa matano kwa wakati mmoja maarufu kama Pentavalent Vaccine

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!