FAIDA ZA MATUMIZI YA ASALI MWILINI

 ASALI

• • • • •

FAIDA ZA MATUMIZI YA ASALI MWILINI


1. Asali hutoa kiwango kikubwa cha virutubisho mbali mbali mwilini mfano;


Kijiko kimoja cha asali, sawa na gram  21 kinatoa Calories 64, Pamoja na Gram 17 za sukari iliyopo kwenye mfumo mbali mbali kama vile; Glucose, sucrose,maltose, na Fructose


2. Asali huweza kupunguza uwezekano wa mtu kushambuliwa na magonjwa mbali mbali kama vile; Stroke, kansa, magonjwa mbali mbali ya moyo kama vile shambulio la moyo yaani heart attack n.k


3. Matumizi ya asali huboresha afya ya macho ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwezo wa macho kuona vizuri


4. Matumizi ya sukari ya viwandani kwa mgonjwa wa kisukari hasa type 2 huwa ni hatari kuliko matumizi ya asali, japo vyote hutakiwa kutumiwa kwa tahadhari kubwa



5. Matumizi ya asali huweza kusaidia kushusha presha ya mwili kutokana na kuwa na antioxidants ndani yake, hali ambayo huweza kuwa msaada pia kwa mgonjwa wa Presha



6. Pia asali husaidia sana katika kuponyesha vidonda mbali mbali kwa haraka, kama vile kwa mtu aliyeungua n.k


7. Matumizi ya asali husaidia katika kupunguza kiwango cha lehemu mwilini


8. Pia wengine hutumia asali kwa matatizo mengine kama vile ya meno, mafua n.k


9. Asali husaidia pia kwa mtu mwenye matatizo ya kuvimba kooni


10. Asali husaidia kwa watu wenye shida ya mvurugiko wa tumbo ndani ya muda mfupi


11. Asali husaidia kuondoa hali ya kichefuchefu na kutapika


12. Matumizi ya asali mara kwa mara husaidia sana kuimarisha kinga yako ya mwili


N.K


Matumizi ya Asali kuponya vidonda SOMA hapa.!!


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!