FAIDA ZA ULAJI WA TENDE MWILINI(tips za afya bora)

 TENDE

• • • • • •

FAIDA ZA ULAJI WA TENDE MWILINI(tips za afya bora)


Tende zinafaida nyingi sana kwenye mwili wa binadamu na hizi hapa ni baadhi ya faida za tende mwilini;


- Tende husaidia katika kuimarisha uwezo wa kuona na kusaidia kwa watu wenye matatizo ya kushindwa kutofautisha rangi


- Tende huweza kukukinga na aina mbali mbali za kansa kama vile; kansa ya tumbo n.k


-  Tende pia husaidia sana kwenye swala zima la Afya ya uzazi kwa wanaume ikiwa ni pamoja na tatizo la nguvu za kiume


- Tende husaidia kuongeza uzito wa mwili kwa kasi hivo kusaidia sana kwa watu waliokonda na wenye tatizo la uzito mdogo kupita kiasi


- Tende pia husaidia sana kwa watu ambao wana matatizo mbali mbali ya choo kama vile; Kukosa choo kabsa, au kupata choo kigumu n.k


- Tende ni chanzo kizuri sana cha madini ya chuma hivo ulaji wa tende kwa wingi husaidia sana kuongeza madini aina ya chuma mwilini


- Tende husaidia kwa watu wenye tatizo la damu kuwa ndogo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Anemia kutokana na kutoa kiwango kikubwa cha madini chuma


- Tende husaidia sana katika kuimarisha mfumo mzima wa chakula ikiwa ni pamoja na kurahisisha umeng'enyaji wa chakula


- Tende husaidia sana kuupa mwili nguvu ya kutosha kutokana na kuzalisha kiwango kikubwa cha sukari katika mifumo mbali mbali kama vile sucrose,glucose n.k


- Tende pia hutoa aina mbali mbali za vitamins mwilini kama vile; Vitamin B1, Vitamin C n.k




KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!