Hirsutism
• • • • •
HALI YA MWANAMKE KUWA NA NYWELE NYINGI USONI(Hirsutism)
Hirsutism hii ni hali ya mwanamke kuwa na nywele nyingi maeneo ya usoni,kifuani,mgongoni,tumboni chini,kwenye mapaja n.k
CHANZO CHA HALI HII;
- mwanamke kuwa na kiwango kikubwa cha hormone aina ya Androgen
- Tatizo la Polycystic ovary syndrome(PCOS)
- mwili kuwa katika mazingira ya kiwango kikubwa cha hormone ya Cortisol ambayo hutokana na;
• Tezi la andrenaline (andrenal gland) kuzalisha kiwango kikubwa sana cha Cortisol
• matumizi ya dawa kama prednisone kwa muda mrefu
- mwanamke kuzaliwa na tatizo kwenye tezi la adrenaline yaani congenital adrenal hyperplasia ambapo huhusisha uzalishaji wa kiwango kikubwa sana cha hormone jamii ya Steroids kama vile; androgen na Cortisol
- Uvimbe kwenye tezi la adrenaline
- Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile; Danazol, Minoxidil n.k
DALILI ZA HALI HII YA Hirsutism NI PAMOJA NA;
✓ mwanamke kuwa na nywele nyingi maeneo ya usoni,kifuani,mgongoni,tumboni chini,kwenye mapaja n.k
✓ wengine huanza kuwa na kipara
✓ Matiti kuwa madogo sana kupita kawaida
✓ kuongezeka kwa misuli ya mwili
✓ Kinembe yaani Clitoris kuwa kikubwa zaidi
N.k
MATIBABU YA HALI HII
- Hali hii huhusisha matibabu ya aina mbali mbali kama vile; matumizi ya dawa
mfano; combined oral contraceptives(COC's), dawa zinazozuia uzalishwaji wa androgeni yaani Anti-androgen drugs, Topical cream kama Vaniqa n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!