KORODANI
• • • • •
IDADI YA KORODANI KWA WANAUME(soma kujua)
Idadi kubwa ya wanaume wana Korodani mbili, lakini sio wote wapo hivo,
Kuna wanaume wana korodani moja tu hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama MONORCHISM,
Lakini pia Kuna idadi chache ya wanaume ambao wana korodani zaidi ya mbili, yaani kuanzia Tatu, Nne n.k hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama POLYORCHIDISM
JE KUNA MADHARA YOYOTE KWA MWANAUME AKIWA NA KORODANI MOJA AU ZAIDI YA MBILI?
- Hakuna madhara yoyote ya kiafya kwa mwanaume mwenye hali hii, japo kuna baadhi ya tafiti chache ambazo zimeonyesha kwamba,
1. Kwa wanaume ambao wana Korodani zaidi ya mbili huwa katika hatari ya Kupata Kansa au Saratani ya Korodani
2. Na kwa wanaume wenye korodani moja huwa katika hatari ya kupata tatizo la Hernia
JE HALI HII HUWEZA KUATHIRI AFYA YA UZAZI KWA WANAUME?
✓ Hapana, hakuna uhusiano wowote kati ya idadi ya korodani na afya ya uzazi kwa mwanaume,
Hivo basi mwanaume huyu atakuwa kama wanaume wengine kwa upande wa uzalishaji mbegu,nguvu za kiume, uwezo wa kumpa mwanamke mimba N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!