JE KUNA MADHARA YOYOTE ENDAPO MAMA MJAMZITO AKIFANYA MAPENZI?

 MJAMZITO

• • • • •

JE KUNA MADHARA YOYOTE ENDAPO MAMA MJAMZITO AKIFANYA MAPENZI?


Majibu; Kabla ya kujibu swali hili,naomba niambatanishe na swali lingine ambalo watu wengi sana wamekuwa wakiniuliza,ili nitoe ufafanuzi kwa pamoja.


1. Je kuna madhara yoyote endapo mama mjamzito atafanya mapenzi?


2. Je kuna madhara yoyote kwa mtoto au mama mwenyewe,endapo hakuna tendo la ndoa kipindi cha ujauzito?


MAJIBU;


✓ Hakuna madhara yoyote kwa mtoto au mama mwenyewe,endapo hatashiriki kabsa tendo la ndoa kipindi chote cha Ujauzito


✓ Hakuna madhara endapo mama atafanya mapenzi akiwa mjamzito, ila kuna angalizo;


ANGALIZO- endapo mama ana historia ya matatizo mbali mbali wakati wa ujauzito kama vile; Mimba kutoka zenyewe, Shingo ya kizazi kulegea na kushindwa kuhimili ujauzito,damu kushindwa kuganda yaani coagulopathy n.k,


Sio salama sana kwa mama kama huyu kufanya mapenzi akiwa mjamzito,kwani huweza kupelekea kupatwa na matatizo kama haya kwa mara nyingine.


MAMA MJAMZITO AZINGATIE HAYA;


- kufanya mapenzi endapo hana tatizo lolote lile wakati wa ujauzito ni salama


- Apende kulala ubavu, hasa ubavu wake wa kushoto kuliko kulalia mgongo


- Asivae nguo za kumbana sana, viatu virefu,mikanda tumboni n.k


- Apende kufanya mazoezi mara kwa mara, ujauzito sio ugonjwa,kiasi kwamba muda wote unalala kitandani.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!