JE UNAWEZA KUBEBA MIMBA MARA TU BAADA YA KUJIFUNGUA?

 MIMBA

• • • •

JE UNAWEZA KUBEBA MIMBA MARA TU BAADA YA KUJIFUNGUA?


Je mwanamke anaweza kubeba mimba nyingine mara tu baada ya kujifungua?


Watu wengi hawajui kwamba mwanamke huweza kubeba mimba nyingine muda mfupi tu baada ya kujifungua, Soma hapa.!!!


Swala la mwanamke kubeba mimba hutegemea na mzunguko wake wa hedhi, endapo mzunguko wa hedhi umerudi kama kawaida, mwanamke huweza kubeba mimba tena,


Na kwa bahati mbaya wanawake wengi baada ya kujifungua husubiri kwanza mpaka waone siku zao za hedhi,ndyo waanze kuchukua tahadhari,


Bila kujua kwamba kupata hedhi ni matokeo ya yai kutokurutubishwa, hivo yai hutoka kwanza ndipo baadae uone siku za hedhi


Endapo mzunguko wako wa hedhi umerudi kama kawaida na yai likatoka,urutubishaji huweza kufanyika na hata usione hiyo hedhi ambayo unaisubiria ili ndyo uanze kuchukua tahadhari


Hivo unaweza kubeba mimba nyingine hata kabla hujaona hedhi tena.


Chukua tahadhari kuepuka mimba sizizotarajiwa


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!