KWANINI SINDANO HUONEKANA TIBA BORA NA YA HARAKA KULIKO VIDONGE?

 SINDANO

• • • • •

KWANINI SINDANO HUONEKANA TIBA BORA NA YA HARAKA KULIKO VIDONGE?


Hili ni swali ambalo baadhi ya watu wamekuwa wakiniuliza sana, na hapa ndyo ufafanuzi wake;


Licha ya kwamba kuna baadhi ya dawa zingine ambazo huwezi kuzipata kabsa kwenye Mfumo wa vidonge bado sindano ni tiba ambayo hutoa matokeo ndani ya muda mfupi sana kwa Mgonjwa au Ugonjwa wowote.


Ukweli ni kwamba ili dawa itoe matokeo lazima ifike sehemu ilipokusudiwa kufika, hapa nitatoa mifano miwili(dawa ya kidonge na dawa ambayo hutolewa kwa njia ya Sindano)


• Dawa ambayo hutolewa kwa njia ya kidonge huweza kuchukua mzunguko mrefu zaidi kufika ilipokusudiwa na matokeo yake ya kufanya kazi kuanza kuonekana yakachukua muda pia


• Dawa ambayo hutolewa kwa Njia ya sindano hutoa matokeo kwa haraka sana ndani ya muda mfupi kwani hufika sehemu ilipokusudiwa kwa haraka zaidi


Mfano; Kama mtu kachomwa sindano matakoni, kwenye paja, au kwenye mkono, Yaani sindano inayochomwa kwenye msuli au kwa kitaalam tunaita Intramuscular(IM) injection hutoa matokeo kwa haraka zaidi kuliko vidonge


- Na Mtu ambaye kapewa dawa kwa njia ya kuchomwa sindano kwenye mshipa yaani kwa kitaalam Intravenous(IV) Injection husababisha kutoa matokeo ya haraka sana kuliko aina nyingine yoyote ya mtu kupewa dawa,


Kwani dawa hiyo ambayo imetolewa hufika moja kwa moja kwenye damu kwa muda huo huo ambao mtu kapewa dawa.


Ndyo maana hata mgonjwa akizidishiwa dose ya dawa ambayo kapewa kwa Njia hii ya kupitishia kwenye mshipa,madhara yake huanza kuonekana ndani ya muda mfupi sana, na nihatari kuliko aina nyingine yoyote ya mgonjwa kupata dawa.


Nimatumaini yangu wale ambao walikuwa wananiuliza sana maswali kuhusu hili, angalau watakuwa wamepata picha na kuelewa kuhusu dawa ambayo hutolewa kwa Njia ya sindano pamoja na vidonge,


pamoja na jinsi dawa ambayo hutolewa kwa njia ya sindano hutoa matokeo kwa haraka zaidi kuliko vidonge.


ANGALIZO; Pia inategemea na aina ya dawa ambayo mgonjwa anapewa


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!