UZAZI
• • • • • •
KWANINI TUNASHAURI MWANAMKE KUBEBA MIMBA KABLA YA MIAKA 35
UMRI MKUBWA (MIAKA 35 NA KUENDELEA)
Inajulikana kwamba kadiri umri wa mwanamke unavozidi kwenda basi uwezo wa kupata mtoto hupungua.
Hii inatokea kwa sababu ya utaratibu uliopo wa mayai kupungua na kuzeeka (Oocyte aging) ambao hupelekea kupungua kwa ubora na wingi wa mayai.
Hali hii iko hivi mtoto wa kike wakati wa mimba yake na mimba ikiwa na umri wa wiki 18 hadi 22 anakua na mayai yapatayo milioni 7, ambayo yanaedele kupungua (attrition) na mtoto wa kike anapozaliwa anakua na mayai yapatayo milioni 2, mayai yanaendelea kupungua na mpaka anafikia kuvunja ungo anakua amebakia na mayai yapatayo 300,000.
Soma: Chanjo Zote za Mtoto toka anazaliwa mpaka umri wa miaka Mitano
Upunguaji na upoteaji wa mayai hua wa kasi sana mwanamke anapofikia umri wa miaka 30 na kuendelea.unywaji wa pombe,uvutaji wa sigara,madawa ya saratani yanaongeza pia kasi ya upoteji wa mayai.
Mwanamke mwenye umri mkubwa anaweza akaendelea kupevusha mayai ila akashindwa kupata mimba kutokana na uchovu wa mayai na mayai kukosa ubora
cc: Dr. mathew
Soma: Chanjo Zote za Mtoto toka anazaliwa mpaka umri wa miaka Mitano
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!