MABADILIKO AMBAYO HUTOKEA MWILINI WAKATI UMELALA USIKU

  USIKU

• • • • •

MABADILIKO AMBAYO HUTOKEA MWILINI WAKATI UMELALA USIKU


Mwili hupata mabadiliko mengi sana wakati ukiwa umelala usiku, na mabadiliko hayo ni pamoja na;


• Kuongezeka uzalishaji wa vichocheo vingi mwilini hutokea wakati wa usiku ukiwa umelala, vichocheo hivo ni kama vile; Melatonin,


• Kupungua kwa kiasi kikubwa kwa kichocheo cha Cortisol ambacho hudhibithi kiwango cha msongo wa mawazo au maarufu kama Stress hormones 


• Misuli mingi ya mwili wako hupumzika wakati ukiwa umelala


• Kinga ya mwili huimarika zaidi kwa mtu anayepata muda wa kutosha wa kulala pamoja na kufanya kazi vizuri sana wakati wa usiku.


Mfumo wa kinga ya mwili wako huzalisha proteins ndogo ndogo maarufu kama Cytokines ambayo husaidia kudhibithi uvimbe, kuponyesha vidonda au majeraha kwa haraka zaidi pamoja na kupambana na mashambulizi ya magonjwa mbali mbali yaani disease's Infection wakati wa usiku ukiwa umelala.


• Ubongo wako huzalisha hormone inayojulikana kama ANTI-DIURETIC HORMONE(ADH) ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha mkojo ukiwa umelala tofauti na wakati wa mchana,


ndyo maana unaweza kulala hata usiku mzima bila kumka na kukojoa hata mara moja,kitu ambacho ningumu sana kutokea wakati wa mchana.


• Umeng'enyaji wa chakula huweza kupungua kwa kiasi kikubwa ukiwa umelala,huku mwili ukitumia sana kiwango cha glucose ambacho umekipata wakati wa mchana katika kuongeza nguvu kwenye mifumo mbali mbali ya mwili,


Kama vile inayohusika na kurepair seli zilizojeruhishwa,kufa n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!