FANGASI
• • • • •
MADHARA YA MASHAMBULIZI YA FANGASI MWILINI
Madhara yanayosababishwa na fangasi mwilini hutegemea na aina ya fangasi pamoja na eneo ambalo fangasi wameshambulia,
Kuna aina mbali mbali za mashambulizi ya fangasi kama vile;
• Kuna fangasi wa kwenye ubongo
• kuna fangasi wa kooni
• kuna fangasi wa kwenye damu
• kuna fangasi wa kwenye ulimi na mdomoni
• kuna fangasi wa sehemu za siri(wanaume&wanawake)
• kuna fangasi wa kwenye kucha
• kuna fangasi wa miguuni
• Kuna fangasi wa mikononi
• Kuna fangasi wa kichwani
N.k
MADHARA YA MASHAMBULIZI YA FANGASI MWILINI NI PAMOJA NA;
1. kusababisha sehemu mbali mbali za mwili kuoza kama mashambulizi ya Fangasi kwenye vidole vya miguuni,kwenye kucha n.k
2. Kusababisha vidonda pamoja na michubuko ya ngozi, mfano mashambulizi ya fangasi wa sehemu za siri kama vile Candida Albicans,mashambulizi ya fangasi wa mdomoni pamoja na Fangasi wa kwenye Ngozi
3. Kusababisha vifo, Mfano mashambulizi ya Fangasi wa kwenye ubongo huua kwa haraka zaidi
4. Kusababisha mtu kushindwa kula kitu chochote, mfano mashambulizi ya fangasi wa kooni ambao huweza kusababisha mtu kupata shida sana ya kumeza chakula,
Pamoja na mashambulizi ya Fangasi Tumboni ambao huathiri hata umeng'enyaji wa chakula
5. Kusababisha tatizo la Miwasho ya mara kwa mara, Mfano mashambulizi ya Fangasi wa sehemu za siri pamoja na Fangasi wa kwenye Ngozi
6. Kusababisha mtu kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya,wenye rangi na mzito kama maziwa mgando, Mfano mashambulizi ya fangasi ukeni jamii ya Candida Albicans
7. Pia fangasi sugu huweza kuathiri hata uwezo wa mwanamke kushika mimba, mzunguko wake wa hedhi N.k
Kujua zaidi KUHUSU tatizo la FANGASI UKENI soma hapa..!!
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!