Ticker

6/recent/ticker-posts

MADHARA YA MTOTO MDOGO KULA MCHANGA AU UDONGO



 MTOTO

• • • • •

MADHARA YA MTOTO MDOGO KULA MCHANGA AU UDONGO


Mchanga au udongo huwa na uchafu wa kila aina kama vile; vinyesi vya binadamu,wanyama, mikojo yao, pamoja na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Minyoo pamoja na bacteria wengi hasa mchanga ukiwa una unyevu unyevu au maji maji.


Hivo athari kubwa ya kula mchanga au udongo kwa mtoto au hata kwa watu wazima kama wakina mama wajawazito hutokana na uchafu uliopo ndani yake pamoja na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama Minyoo na Bacteria



MADHARA YA MTOTO MDOGO KULA MCHANGA NI PAMOJA NA;


- Mtoto kuanza kutapika mara kwa mara


- Mtoto kuharisha mara kwa mara


- Mtoto kukosa kabsa hamu ya kula chakula


- Mtoto kuwa na homa za mara kwa mara


- Mtoto kupatwa na tatizo la kuumwa na tumbo mara kwa mara


- Lakini pia endapo mtoto hupenda kula kiasi kikubwa cha mchanga kwa wakati mmoja huwa katika hatari ya kupata tatizo la utumbo kuziba yaani kwa kitaalam tunaita Intestinal Obstruction


Ukiona dalili kama hizo kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya Tiba kwa mtoto


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments