MAGONJWA YANAYOSABABISHA KUZIBA KWA HEWA PAMOJA NA MATATIZO YA UPUMUAJI(chronic obstructive pulmonary disease or COPD)

   MAGONJWA

• • • • • •

MAGONJWA YANAYOSABABISHA KUZIBA KWA HEWA PAMOJA NA MATATIZO YA UPUMUAJI(chronic obstructive pulmonary disease or COPD)


Hapa tunazungumzia mjumuisho wa magonjwa yote ambayo huziba mfumo wa hewa pamoja na kuleta matatizo ya upumuaji kwa mgonjwa ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Chronic obstructive pulmonary disease au  kwa kifupi COPD.


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA SHIDA HII NI PAMOJA NA;


- Wavutaji wa sigara


- Watu wenye tatizo la Asthma


- Watu ambao wana mgonjwa wa shida hii katika familia yao


- Watu ambao wanapatwa na vumbi kwa muda mrefu kutokana na kazi wanazofanya


- Watu ambao wanapatwa na moshi kwa muda mrefu,uwe moshi wa magari,moshi ya kuni n.k


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA


- Mtu kupiga chafya mara kwa mara


- Kupata shida sana ya upumuaji


- Kutoa sauti wakati wa kuvuta na kutoa hewa(wheezing)


- Kupata maumivu makali ya kifua


- Kuchoka sana 


- Kukohoa kikohozi ambacho hakiishi


- Kukohoa damu,usaha au makohozi ambayo yana rangi kama njano N.k


- Kupata shida ya Kuvimba sana miguu


- Uzito wa mwili kupungua sana kwa kasi

N.k


MATIBABU YA SHIDA HII


- yapo matibabu mbali mbali kama vile; matumizi ya bronchodillators, antibiotics mbali mbali pamoja na vitu vya kuepuka kama Sigara, mazingira yenye vumbi,moshi n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!