Ticker

6/recent/ticker-posts

MAMBO YA KUFANYA BAADA YA KUOVERDOSE DAWA YOYOTE



 OVERDOSE

• • • • • •

MAMBO YA KUFANYA BAADA YA KUOVERDOSE DAWA YOYOTE


Watu wengi hupaniki sana baada ya kugungua wametumia dawa kupita kiwango cha kawaida au Overdose dawa mbali mbali,


Je ufanyeje baada ya kugundua umejioverdose dawa?


MAMBO YA KUFANYA BAADA YA KUOVERDOSE DAWA YOYOTE


✓ Kwanza kabsa unaweza usikumbuke kwamba kiwango cha dawa ulichotumia ni sahihi au sio sahihi, ila kuna baadhi ya dalili ambazo huweza kukuonyesha kwamba umejioverdose dawa baada ya kutumia ndani ya muda flani kama vile;


- Kuanza kuona maruerue


- Kupata kizunguzungu kikali


- Kuanza kupata dalili kama za kuchanganyikiwa au hallucinations


- Kuanza kupata kichefuchefu na kutapika sana


- Kupoteza fahamu


- Kushindwa kabsa kutembea


- Mwili kuanza kuishiwa na nguvu gafla


- Mwili kuanza kutetemeka


- Mtu kushindwa kupumua

n.k


✓ Pili inategemea na aina ya dawa na kiwango ambacho umejioverdose, Hivo unashauriwa baada ya kugundua kwamba umejioverdose dawa kuwahi hospital ili upate msaada,


Kwani wataalam wa afya ndyo watajua aina ya dawa, kiwango na madhara yake mwilini na kukupatia tiba kulingana na tatizo lako


✓ Japo wengine hukimbilia kwanza njia za asili kama kutumia maziwa, dawa mbali mbali za kumtapisha mtu n.k


Unashauriwa baada ya kufanya hivi bado uende hospital kwa sababu hutajua kama sumu ya dawa bado ipo au imeisha na haitaleta madhara tena kwa hapo baadae.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments