MASHAMBULIZI YA AMIBA(AMOEBA) KWENYE UBONGO

 AMIBA

• • • • •

MASHAMBULIZI YA AMIBA(AMOEBA) KWENYE UBONGO


Mashambulizi haya husababishwa na Amoeba jamii ya NAEGLERIA FOWLERI ambao husafiri kupitia puani na kuelekea kwenye ubongo, kisha kusababisha uharibifu mkubwa wa Ubongo.


Mashambulizi ya Amiba au amoeba kwenye ubongo ni moja ya mashambulizi hatari na ambayo husababisha kifo,


DALILI ZA MGONJWA ALIYESHAMBULIWA NA AMOEBA KWENYE UBONGO NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa kupatwa na tatizo la mwili kutetemeka au Seizures


- Mgonjwa kulala sana


- Tatizo la shingo kukakamaa


- Uwezo wa mtu kunusa na kujua harufu au kujua ladha ya kitu mdomoni kubadilika


- Pua kubana au kuanza kutoa maji maji


- Kupata kichefu chefu pamoja na kutapika


- Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na Homa


- Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa


- Mgonjwa kupata dalili kama za mtu kuchanganyikiwa


- N.k


MATIBABU YA MASHAMBULIZI YA AMOEBA KWENYE UBONGO


✓ Mashambukizi haya hutibiwa kwa kutumia mjumuisho wa dawa mbali mbali kama vile;


• Amphotericin B


• Miltefosine


• Dawa  mbali mbali jamii ya antibiotics pamoja na dawa za fangasi yaani Antifungal Drugs


KUJUA ZAIDI kuhusu Ugonjwa wa AMIBA soma hapa..!!!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!